Na; John Walter-Simanjiro

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 Sahil Geraruma  amesema kuna kila sababu kwa Watanzania kuendelea kupanda miti katika maeneo mbalimbali ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.


Geraruma ametoa wito huo wakati akizungumza na walimu na wanafunzi Katika shule ya Sekondari Mgutwa iliyopo Kata ya Shambarai tarafa ya Moipo wilayani Simanjiro mkoani Manyara alipotembelea Mradi wa upandaji miti na utunzaji wa Mazingira.Kwa mujibu wa Mkuu wa shule ya Sekondari Mgutwa Donald Lema amesema gharama za Mradi huo ni shilingi Milioni 18,210,000.


Ameeleza kuwa lengo la Mradi ni  kutunza mazingira ya shule na kuchangia juhudi za Serikali Katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambapo jumla ya miti 2,150 imepandwa na inaendelea vizuri.


Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 unahimiza Wananchi kujitokeza Katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi itakayofanyika mwezi Agosti 23.


Share To:

JUSLINE

Post A Comment: