Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Mwaka 2022, Sahili Geraruma Ameiagiza Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha pamoja na wataalamu katika halmashauri za mkoa huo kuhakikisha wanatumia namna bora ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye lengo la kuzisaidia jamii.

ametoa maagizo hayo wilayani Monduli wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika shule mpya ya sekondari Mswakini huku akisisitiza wataalamu wa Halmashauri kusimamia vema wakandarasi wanao tekeleza miradi ya Serikali katika maeneo yao.


Ukaguzi pamoja na kuzinduliwa miradi ya maendeleo kwa wananchi na Mwenge wa Uhuru mkoani Arusha unaendelea ikiwa ni kuhakikisha thamani halisi ya fedha inaonekana na huduma iliyokusudiwa inaifikia jamii Kwa wakati.

Hata hivyo kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amemtaka mkandarasi anaye tekeleza mradi wa shule ya sekondari ya Mswakini kuyafanyia kazi mapungufu yote yaliyo jitokeza haraka iwezekanavyo.

kwa Upande wake Mkuu wa wilaya ya Monduli Frank Mwaisumbe amesema amepokea maelekezo ya Mwenge wa Uhuru na ipo tayari kuyafanyia kazi.


Share To:

Post A Comment: