Mtandao namba moja kwa utoaji wa huduma za kidigitali nchini Tanzania Tigo Leo June 5 , 2022 umetangaza rasmi kushiriki maonyesho Ya Biashara Ya Utalii Ya Kili Fair  " KILI FAIR 2022 ".

Akizungumza katika Maonyesho hayo mwakilishi kutoka Tigo amesema kuwa

" NI FURAHA YETU kuhakikisha kuwa malipo kidigitali YANARAHISISHWA popote utakapo kuwa. Tigo Pesa kwa kushirikiana na DPO Pay @dpo_group tumerahisisha malipo mbalimbali kwa wateja wetu.

Tutaendelea kushirikiana ili kumrahisishia zaidi mteja wetu popote alipo.

Karibu wote KARIBU-KILIFAIR 2022 Tuko katika Maonyesho Ya Biashara Ya Utalii Ya Kili Fair kukuonesha huduma na bidhaa za kipekee zitakazokusaidia kuishi maisha ya kidigitali.

Tembelea Banda la Tigo viwanja vya Magereza, Arusha ujionee huduma na bidhaa za kidigitali kwa ajili yako " . Alimalizia .

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: