Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka akifungua mkutano wa tatu wa Kamati Tendaji ya Mradi Jumuishi wa Kupambana na Ujangili na Biashara haramu ya Wanyamapori Tanzania uliofanyika Ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka amefungua mkutano
wa tatu wa Kamati Tendaji ya Mradi Jumuishi wa Kupambana na Ujangili na
Biashara haramu ya Wanyamapori Tanzania.
Mradi wa
huo unalenga kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na ujangili na
biashara haramu ya wanyamapori.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mkutano huo leo Juni 27, 2022 uliofanyika katika Ofisi za
Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma, Prof. Sedoyeka amesema kuwa lengo
la mkutano huo ni kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi na kutoa mwongozo
kwa Kitengo cha Usimamizi wa Mradi ili kifanye kazi kikamilifu kufikia lengo la
Serikali la kutokomeza ujangili ifikapo mwaka 2025.
Amesema
Wizara ya Maliasili na Utalii inasimamia ushirikiano kati ya washirika na wadau
katika utekelezaji wa mradi huo ili kufikia dira ya Sera ya Taifa ya
Wanyamapori inayolenga kulinda wanyamapori na makazi yao, usimamizi na
maendeleo ya rasilimali za wanyamapori na kuzuia matumizi haramu ya
wanyamapori.
Aidha,
Prof. Sedoyeka amesema kuwa mradi huo ulilenga pamoja na mambo mengine, kupitia
Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Ujangili na Mkakati wa Usimamizi wa Maeneo
ya Wanyamapori, kupitia kanuni za uwindaji wa Kitalii, kuwajengea uwezo
watumishi katika kupambana na ujangili, kuwezesha wananchi katika kupambana na
wanyamapori wakali na waharibifu na kuboresha maisha yao kwa kushiriki katika
usimamizi wa wanyamapori.
Pia
amefafanua kuwa mradi umefanikiwa kununua Land cruiser Hard top kumi (10) mpya
ili kusaidia utekelezaji wa mikakati ya kukabiliana na ujangili na biashara
haramu ya wanyamapori.
Mkutano
huo umehudhuriwa na Amon Manyama kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo Duniani (UNDP), Wajumbe wa Kamati ya
Uendeshaji wa Mradi na Kitengo cha Usimamizi wa Mradi.
Post A Comment: