Na Elizabeth Joseph, Monduli.


Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli wanatarajia kuanza kutumia Jengo jipya la Utawala mwishoni mwa mwaka huu 2022 ambalo hadi kukamilika litagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 2.


Hayo yamesemwa na Kaimu Mhandisi Ujenzi Wilaya ya Monduli,Mhandisi Lugano Mwakalinga wakati wa mahojiano juu ya ujenzi wa jengo hilo ambalo lilianza kujengwa mnamo Aprili 29 2021 huku likiwa na jumla vyumba vya ofisi 63 za Idara mbalimbali pamoja na Ukumbi wa mikutano.


"Kazi hii inafanyika kwa njia ya Force account na hadi sasa tumetumia Milioni 750 ya ujenzi ulipofikia ambapo phase ya kwanza ilikuwa ni msingi kwa kusuka nondo,nguzo pamoja na kumwaga jamvi............


"Phase ya pili tulianzia level ya jamvi na kuset nguzo zote ambazo jumla ziko 157,kupiga kuta kwa tofali, nguzo mlalo na nguzo za floor ya kwanza ili kubeba upauzi wa jengo"aliongeza Mhandisi Mwakalinga.


Alieleza kuwa Milioni 750 zilizobaki zinatarajiwa kufanya shughuli za upauzi wa jengo hilo ikiwa ni pamoja na kutandika vigae na kuweka fremu za milango.


Alibainisha kuwa serikali imechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi huo ambapo hadi sasa imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 1 na Milioni 500 huku bado wakihitaji shilingi Bilioni 1 na Milioni 135 ili kukamilisha ujenzi huo ambazo alisema tayari wako kwenye utaratibu wa kuandaa nyaraka za kuomba fedha hizo.


Mwisho.

Share To:

Post A Comment: