MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa siku ya Wellness Day iliyoanzishwa na Benki ya CRBD ikiwa ni maalumu kwa ajili ya wafanyakazi kushiriki katika michezo lengo likiwa ni kutafakati na kuthamini mchango wa wafanyakazi kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa ,Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo na kulia ni Meneja wa CRDB Tanga January
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa siku ya Wellness Day iliyoanzishwa na Benki ya CRBD ikiwa ni maalumu kwa ajili ya wafanyakazi kushiriki katika michezo lengo likiwa ni kutafakati na kuthamini mchango wa wafanyakazi kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa ,Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo na kulia ni Meneja wa CRDB Tanga January
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa akizungumza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo


Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo akizungumza wakati wa halfa hiyo




NA OSCAR ASSENGA, TANGA

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amesema miongoni mwa wahanga wakubwa wa magonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo Presha na Kisukari na mengine ni wafanyakazi kwa sababu siku zote wamekuwa na maisha yanayotabirika.

Mgandiliwa aliyasema hayo wakati wa siku ya Wellness Day iliyoanzishwa na Benki ya CRBD ikiwa ni maalumu kwa ajili ya wafanyakazi kushiriki katika michezo lengo likiwa ni kutafakati na kuthamini mchango wa wafanyakazi .

Ambapo waliona ni bora waanzishe siku hiyo maalumu ya kuwasaidia na kuleta furaha kwa wafanyakazi na kuona jinsi gani wanaweza kuweka uwiano sawa kati ua maisha ya kazi na maisha binafsi ili kazi isijekuwa adhabu

Umuhimu wa siku hiyo unatokana na kwamba wamekuwa wakifanya kazi kwa siku zote 365 kasoro siku ya Krismas na Eid kwa kutokana na hilo benki hiyo ilikuja ikafikiria, kutafakati na kuthamini mchango wa wafanyakazi na kuona bora ianzishe mpango huo.

Alisema kwani asubuhi wanaingia kazini wakimaliza wanakula na kulala na siku inayofuatia wanaendelea na kazi hivyo maisha yao yana mzunguko huo kupitia huko miili inakuwa dhaifu sana kinga zinakuwa zimeshuka kwa kiwango kikubwa kutokana na aina ya maisha wanayoishi.



“Leo hii magonjwa kama vile Presha,Kisukari yanaongezaka kwa kiwango kikubwa tatizo hatufanyia mazoezi..ukiona mtu anaamka asubuhi anaenda ofisini muda wa kula anaondoka na akirudi anaendelea na shughuli zake na mwisho wa siku hawana muda ma mazoezi anatoka ofisi wanarudi nyumbani wamechoka anaoga anakula na kulala”Alisema DC Mgandilwa.

Mkuu huyo wa wilaya alisema jambo ambalo wamelifanya kwake ni sehemu ya shughuli ndani hivyo isipokuwa kuna maboresho wanatakiwa kuyafanya wakati mwengine .

“Niwaambie tu kwamba idara iliyoratibu sio vibaya wakaendelea kwenye matawi yao kwa kuweka vyumba vya mazoezi kuwawezesha wafanyakazi waweze kushiriki kwenye mazoezi lakini tofauti na hapo tutaishi kukuta na na kutimiza wajibu”Alisema DC Mgandiliwa.

Hata hivyo alisemaq benki hiyo imekuwa mmoja wa wabia wakubwa sana wa Serikali kwa kujitolea hivyo nao wataendelea kuwahaidi kuwa kushirikiana nao bega kwa bega ikiwemo kuendelea kufungua milango

Awali akizungumza Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Benki ya CRDB Chiku Issa alisema Siku ya Wellness Day ya Benki hiyo ilianzishwa miaka miwili iliyopita bahati mbaya watu wa Kanda ya Kaskazini wanaifanya kwa mara ya kwanza kwa sababu hapo nyuma walishindwa kutokana janga la Corona.

Alisema walipoanza kanda hiyo walilazimika kuigawa mara mbili kwa sababu za kijografia na ya kwanza ilifanyika Mkoani Arusha iliyoshirikisha wafanyakazi Manyara,Arusha na Kilimanjaro.

“Tuliona tuigawe mara mbili leo tupo hapa Tanga kwa ajili ya siku hii tupo kuangalia afya na wafanyakazi wa benki kama mnavyojua tunaingia kazini lakini muda wa kutoka hatuna mpaka tuhakikishe vitabu vimebalance ili kuweza kujianda na siku inayofuata”Alisema Meneja huyo wa Kanda ya Kaskazini.

Naye kwa upande wake Meneja wa Rasiliamali Watu wa Benki hiyo wa Kanda ya Kaskazini Cosmas Sadat alisema Tanga wana malengo yao wanaamini kwamba mkoa huo unaweza kuwa Hub ya Kanda ya Kaskazini .

Alisema wamefanya mabadilko madogo ya kuhamisha wafanyakazi kwa ajili ya kuchanganya wanatengeneza ili ziweze kuwa na uwiano sawa na wanataka kila mkoa nguvu zilingane kwa kufanya hivyo kanda hiyo wataweza kuwa wa kwanza.

 







Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: