Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari juu ya fursa ya Sh. Bilioni 20 itakayotolewa kwa waandishi wa watakaoandika maandiko ya utafiti juu ya Jamii duniani kote.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari juu ya fursa ya Sh. Bilioni 20 itakayotolewa kwa waandishi wa watakaoandika maandiko ya utafiti juu ya Jamii duniani kote kulia kwake ni  Neema Tindamanyire,  mratibu wa mabaraza ya Sayansi Kusini mwa Jangwa la Sahara.

NNa Karama Kenyunko 

MABARAZA 11 ya utafiti duniani ikiwemo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) yameweka fedha kiasi cha Euro milioni nane sawa na Sh. Bilioni 20 kwa ajili ya kupata watafiti watakaoandika maandiko ya utafiti katika nyanja mbali mbali ikiwemo mazingira, uchumi endelevu na ustawi wa binadamu.

Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dkt. Amos Nungu amesema hayo leo Juni 27, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya ufadhili huo unaotolewa na nchi 11 za Mabaraza hayo ya Utafiti Duniani.

Amesema shindano hilo ambalo limefunguliwa Mei 15, 2022 na linatarajiwa kufungwa Agosti 28 mwaka huu ni fursa kwa watafiti wa kitanzania ambao ikiwa watajitokeza na kuandika maandiko ya utafiti bora katika maeneo yanayohusu jamii hasa nyanja za Lishe, mifumo ya chakula, nishati na maendeleo ya mijini basi watafanikiwa kupata fedha hizo.

Amesema kati ya nchi hizo 11, Afrika zipo Tanzania, Kenya na Ivorycost huku pia kuna nchi kutoka mabara ya Ulaya, Asia na Amerika Kusini.

Nchi nyingine ni Chile, China, Afrika Kusini, Switzerland, Sweden, Tanzania, Uturuki, Côte d'Ivoire , Kenya, Netherland na Norway.

"Ili kupata fedha hizi watafiti mbalimbali nchini wanaaswa kujitokeza na kuandika maandiko ambayo yatashindanish kutoka maeneo yaliyotajwa duniani yakiwemo ya lishe, nishati na maendeleo ya mijini". Amesema Nungu

Amesema, nchi hizo zimeweka fedha pamoja kwa makubaliano kwamba kila nchi inafadhili watafiti kutoka nchini kwake waunde timu ya pamoja iwe na takribani nchi tatu hizo nchi tatu lazima moja itoke Kusini nyingine Kaskazini,” alisema.

Amesema kikubwa kinachotakiwa katika kuomba ufadhili huo ni umahiri wa kuandika mradi, watafiti watakaofanikiwa nafasi hiyo Costech itaongea na serikali kuongeza fedha kwa sababu kwa watakaoshinda tume hiyo imetenga sh million 120 kwa kila mradi.

Hata hivyo Dkt. Nungu amewataka watafiti kwenda kwenye website ya costech kuangalia fursa iliyopo.
Share To:

Post A Comment: