Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) leo Mei 6, Jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa ya kuhudumia watoto (UNICEF) Ofisi ya Tanzania Dkt. Daniel Baheta na Mkuu wa Sekta ya Elimu UNESCO kwa upande wa Tanzania Faith Shayo kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu elimu kuelekea Mkutano  wa Kimataifa wa Elimu   utakaofanyika mwezi Septemba 2022 nchini Marekani wenye lengo la kuleta mabadiliko Chanya  katika Sekta ya  Elimu.


Katika kikao hicho Waziri Mkenda aliwahakikishia mashirika hayo ushirikiano katika kuleta mageuzi ya elimu nchini.

Share To:

Post A Comment: