WATOTO 56 ambao baadhi yao wazazi wao walikua wanasumbuliwa na ugonjwa wa fistula wamezaliwa salama bila ya matatizo yoyote Katika Hospitali ya CCBRT iliyopo Mkoani Dar es Salaam.


Akizungumza hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali hiyo, Brenda Msangi amesema kuwa, kuzaliwa kwa watoto hao kumetokana na kuboreshwa kwa utoaji wa huduma za afya kwa mama mjamzito na watoto wachanga Ili waweze kuzaliwa salama.

Alisema kuwa, licha ya hospitali hiyo kutoa matibabu ya fistula, lakini pia wameweza huduma bora za afya kwa mama mjamzito na watoto chini ya miaka mitano Ili waweze kupata huduma bora za matibabu.

" Kuna jengo jipya ambalo tumejenga kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakimama wenye fistula, ulemavu na wasichana wanaopata mimba wakiwa na umri mdogo.


" Katika jengo hilo,watoto 56 ambao baadhi yao wazazi wao walikuwa wanasumbuliwa na fistula wamezaliwa salama bila ya matatizo yoyote, hiI Inatoka a na kuboresha huduma za afya kwa mama mjamzito na watoto wachanga Ili waweze kupata huduma bora za matibabu," alisema Msangi.


Aliongeza kuwa, hospitali hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa wajawazito na watoto wachanga Ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na wajawazito wanajifungua salama.

Alisema kuwa, lakini pia watahakikisha wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo wa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali za matibabu, wanaopata huduma bora.

Alibainisha kuwa, katika kuelekea maadhimisho ya siku ya fistula ambayo kitaifa yatafanyika Mei 23 Mkoani Mwanza, CCBRT imejipanga kuboresha huduma za matibabu Kwa wagonjwa hao ili waweze kurudi kwenye hali zao za kawaida.

Hata hivyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Dk. Rashid Mfaume alishukuru hospitali hiyo Kwa kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa mama mjamzito na watoto wanaozaliwa katika hospitali hiyo.

Alisema kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali Ili kuhakikisha wanatoa huduma bora za afya kwa wajawazito na watoto chini ya miaka mitano, jambo ambalo litapunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

" Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kuwa, wajawazito wanajifungua Salama, lengo ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, ndomana tumeboresha huduma, vitendea kazi, wato huduma za afya na matibabu pamoja na mazingira bora Ili wajawazito waweze kujifungua Salama," alisema Dk. Mfaume.


Serikali kupitia Sera ya Afya ya Mwaka ya 2007, ililenga kuboresha afya ya uzazi, mzazi, vijana na mtoto nchini Tanzania ya mwaka 2016-2020 iliweka mazingira wezeshi ya kupunguza magonjwa, vifo vya akina mama na watoto wachanga pamoja na kutoa huduma bora za matibabu.


Mwaka Jana ilisaini utekelezaji wa Mpango wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto(PJT-MMMAM) mpango huo umeanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2021-2026, katika mpango huo pamoja na mambo mengine, umelenga kuboresha utoaji wa huduma bora za afya Kwa wajawazito na watoto kuanzia umri sifuri hadi miaka minane.

Share To:

Post A Comment: