Mbunge wa Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi (Kushoto) akipata maelezo kuhusu tunda la Kweme kutoka kwa Mtafiti na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu wa Chuo Kikuu cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia Cha Nelson Mandela (NM-AIST) Bi . Philipina Shayo (kulia) alipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania leo Mei 18 ,2022 uwanja wa Jamhuri Dodoma.


Wanafunzi wa Dodoma Sekondari (Kushoto) wakimsikiliza Mtafiti na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu wa Chuo Kikuu cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia Cha Nelson Mandela (NM-AIST) Bi . Philipina Shayo (kulia) aliyekuwa akiwaelezea faida zitokenazo na mbegu za tunda la kweme wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania leo Mei 18 ,2022 uwanja wa Jamhuri Dodoma.


Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Msingi Feza ya Jijini Dodoma (Kushoto) wakipata maelezo kuhusu mbegu za tunda la Kweme kutoka kwa Mtafiti na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu wa Chuo Kikuu cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST) Bi . Philipina Shayo (kulia) alipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania leo Mei 18 ,2022 uwanja wa Jamhuri Dodoma.


Wakazi wa Dodoma (Kushoto) wakipata maelezo ya kina kuhusu tunda la Kweme kutoka kwa Mtafiti na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu wa Chuo Kikuu cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia Cha Nelson Mandela (NM-AIST) Bi . Philipina Shayo (kulia) walipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania leo Mei 18 ,2022 uwanja wa Jamhuri Dodoma.


Mwonekano wa Tunda la Kweme na mbegu zake mmea uliofanyiwa utafiti na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu Cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST) Bi . Philipina Shayo katika Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania leo Mei 18 ,2022 uwanja wa Jamhuri Dodoma....................................................

Wananchi wa Jiji la Dodoma wavutiwa na tunda la kweme linalopatikana katika Banda la Chuo Kikuu cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST) leo Mei 18, 2022 kwenye maonyesho ya Wiki ya Ubunifu wa Tanzania yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri.Wananchi hao walifanikiwa kupata maelezo ya kina kuhusu tunda hilo, kutoka kwa Mtafiti na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu kutoka NM-AIST Bi . Philipina Shayo kuwa, mmea huo wa asili utambaao ni jamii ya matango ambapo hulimwa nchini Tanzania katika mkoa wa Tanga, Arusha, Mbeya, Ruvuma,Morogoro, Kilimanjaro na Zanzibar pamoja na nchi jirani za Msumbiji na Uganda.“tunda hili lina uzito kati ya gramu 7 hadi 20 ,likiwa na mbegu au karanga zipatazo 80-200 nadani yake ambazo zikihifadhiwa kwenye mazingira makavu zinaweza kukaa hadi miaka nane bila kupoteza ubora wake" alisema Bi. PhilipinaAlizidi kueleza kuwa, mbegu za tunda la Kweme zina faida nyingi kwa jamii ikiwemo kutumiwa na wakina mama wanaonyonyesha, hutengeneza sabuni, mishumaa na urembo wa ngozi na nywele.Amefafanua zaidi kuwa, tunda hilo hutibu ugonjwa wa Jongo (rheumatism) , hutibu matatizo ya tumbo, husaidia kupunguza hewa ya ukaa ambayo ina madhara kwa binadamu na mazingira .Bi. Philipina ameongeza kuwa, mashudu ya tunda hilo hutumika kutengenezea vyakula vya mifugo pamoja na kuboresha mazingira na udongo hususani kwenye kilimo mseto haswa maeneo ya milimani kama vile Kilimanjaro, Meru na Upare.Aidha Bi. Philipina aliwafafanulia wananachi hao kuwa katika kila mbegu ya kweme yenye uzito wa kilogramu 100 husaidia binadamu kupata mafuta 28%, Protini 25%, Wanga 5%, Asidi ya Mafuta (linoleic acid) 47% pamoja na madini ya Zinki, Selenium, Potasiamu,Fosforasi, Kalsium, Chuma, Sodiam na Magneziamu.Bw.Yusuph Nandonde mwananchi aliyepata fursa ya kutembelea Banda la Nelson Mandela ameeleza kunufaika na elimu aliyoipata kutoka kwa Mtafiti huyo kwa kuwa hapo awali alizoea kuziona na kula mbegu zake bila kulifahamu tunda linalotoa mbegu hizo."Hakika mtembea bure, siyo sawa na mkaa bure nimekuja na nimeondoka na kitu cha thamani sana ,hongereni kwa kutoa elimu hii muhimu kwa jamii yetu alisema" Bw. YusuphChuo Kikuu cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela ni moja ya Taasisi za Vyuo Vikuu iliyoshiriki Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania iliyoanza tarehe 16 Mei 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: