Na Ahmed Mahmoud

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela Amewataka wabunifu mkoani Arusha kutoishia kwenye tafiti waende Mbali zaidi katika kuzalisha kwa wingi ili kuyafikia Masoko ya hapa nchini na nje ya nchi.


Mongela Ameyasema hayo kwenye wiki ya Ubunifu 2022 kwa mkoa wa Arusha ikiwa ni sehemu ya wiki ya Ubunifu nchini itakayofanyika Jijini Dodoma mei 15 mwaka huu inayoenda na kauli mbiu "Ubunifu kwa maendeleo endelevu"


Amesema kwamba ipo haja kwa wabunifu nchini kuacha kujikita katika tafiti pekee na kuanza utengenezaji wa bidhaa walizobuni kwa wingi ili kuyafikia Masoko hilo litakuwa jambo litakalosaidia ukuaji wa maendeleo.


"Niwaombe sana sisi serikali ya mkoa tutatoa eneo kwa ajili ya kufanya mkoa wa Arusha kuwa kitovu Cha Ubunifu nchini ili kuendeleza tafiti ambazo zimeshabuniwa kuweza kuleta tija na kuinua uchumi"


Awali akiongea kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa wiki ya Ubunifu mkoa wa Arusha Mkurugenzi wa program wa MS TCDC Sara Ezra Teri amesema Msingi wa ushiriki wao umejikita katika dhana nzima ya kijana anashiriki vipi katika Ajira na uongozi ili kuweza kuwasilisha kwa serikali katika kusaidia utungaji sera.


Amesema kwa Ubunifu ni sehemu yao ya kusaidia kuandaa vijana ndio maana wameanzisha mafunzo kwa wiki nzima kwa wajasiriamali kutambua wajibu wao kwa Lengo la kukuza Ubunifu.


Kwa Upande wake Collins Kimaro Meneja Mkuu wa Westerwelle startup house Arusha Amewataka wabunifu nchini kushiriki na kujiuliza swali la kauli mbiu ya wiki hiyo kuona wanaibadilisha vipi fikra kuwa fursa za kukuza Ubunifu nchini.


Amesema vijana wengi nchini bado wanaishi kwenye fikra za kijamaa ambazo haziwasaidia kujitambua uelekeo wao wa kukuza uchumi wao hivyo Elimu pekee sio Suluhu ni moyo wa kujitambua na kujitoa katika kuziona fursa za kiuchumi ndio utawasaidia kutimiza ndoto zao. 


wiki ya Ubunifu mkoa wa Arusha imeandaliwa na mashirika 11 ikiwemo MS. TCDC, YouLead Afrika, ANZA Chanya Change, Ndoto Hub IAA Startup business Centre Twende Social Innovation Centre Dot Tanzania Women Innovators for women Entrepreneurs Siverleaf Academy na Westerwelle startup Haus Arusha. 

Wiki ya Ubunifu kitaifa inatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma tarehe 15 mei ikiandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu Sanyansi na Teknolojia na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: