Mgeni rasmi katika mkutano huo katibu tawala wa wilaya ya Arumeru Mwl.James Nchembe aliwataka wananchi hao kushirikiana kwa pamoja uanzishwaji wa aina mpya ya utalii Geopark.

 Na Pamela Mollel,Arusha


Zaidi ya vijiji 12 wilayani Arumeru, mkoani Arusha vimeingizwa kwenye mchakato maalum wa uanzishwaji wa aina mpya ya utalii nchini.

Utalii huu mpya wa kijiolojia, maarufu kama Geopark, unahusisha Zaidi maeneo ya taswira ya nchi kama, milima, mapango, uoto wa asili na maporomoko ya maji, na kwa sasa ndio aina ya utalii unaopendwa sana na wakazi wa nchi za Asia hususan China, Japan na India.

Aina hii mpya ya Utalii wa Kijiolojia unatambulika na kuorodheshwa chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Vijiji vinavyojumuishwa katika uanzishwaji wa utalii wa Geopark, kuuzunguka mlima Meru, ni vile vinavyopakana na hifadhi ya Arusha.

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa shirika la hifadhi za taifa ambaye pia ni Mkuu wa Hifadhi ya Arusha, Albert Mziray anasema kuwa ndani ya vijiji husika kuna vivutio vingi ambavyo vinaweza kuingizwa katika mfumo huo mpya wa Geopark.

“Mfumo huu tunauita mfumo wa Asili wa Mlima Meru, au Mount Meru Natural System,” anaongeza Mziray.

Mziray aliongeza kuwa wanavijiji kupitia aina hii mpya ya Utalii wanaweza kunufaika kutokana na wageni watakaokuwa wanatembelea vivutio vilivyomo ndani ya maeneo yao.

Mkutano huo ulifanyika katika chuo kikuu cha Arusha huku zaidi ya wanavijiji 300 wanapewa elimu ya ufahamu kuhusu aina hiyo mpya ya utalii shirikishi.

Kamishna msaidizi wa uhifadhi, Mkuu wa kitengo cha sayansi ya uhifadhi na mahusiano ya jamii (TANAPA) Godwell Meing’ataki anaongeza kuwa sio kila mtalii hupendelea kuona wanyamapori, baadhi yao wangetaka kuona vivution vingine tofauti ambavyo tayari vinapatikana ndani ya maeneo ya vijiji husika.

Kamishna Msaidizi wa uhifadhi wa shirika la hifadhi za Taifa ambaye pia ni mkuu wa hifadhi ya Arusha,Albert Mziray akizungumza katika mkutano maalumu uanzishwaji wa aina mpya ya utalii Geopark katika chuo kikuu cha Arusha

Kamishna Msaidizi wa uhifadhi ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Sayansi ya uhifadhi na mahusiano ya jamii TANAPA Godwell Meing'ataki
Wananchi zaidi ya 300 wakifatilia mkutano maalumu wa uanzishwaji wa aina mpya ya utalii Geopark

Share To:

Post A Comment: