Hayo yamezungumza na Comredi Raymund Mhenga Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Ruvuma wakati wa Ziara ya Kamati ya utekelezaji ya Uvccm Mkoa huo kwenye kata ya Mtina ,Jimbo la Tunduru Kusini,Wilaya ya Tunduru.
Ziara hiyo ya Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Ruvuma,yenye malengo ya kuwashukuru vijana wa CCM kwa ushirikiano mkubwa waliowapa viongozi hao wa UVCCM Mkoa, lakini kujitoa kwao katika kukipigania chama kwenye shughuli zote za chama ikiwemo chaguzi za marudio ya udiwani,chaguzi za serikali za mtaa, na chaguzi za serikali kuu za mwaka 2020.Pia kuhamasisha Uchaguzi na Sensa ya watu na Makazi inayotegemea kufanyika tarehe 26/08/2022.
Mwenyekiti Mhenga aliwasisitiza Vijana kugombea nafasi mbalimbali kwenye chaguzi hizi ndani ya chama na kuwahaidi kuwa Uvccm itajitahidi kusimamia haki na maslahi ya Vijana hao watakaogombea.Pia mwenyekiti alipongeza kazi kubwa inayofanywa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuleta maendeleo kwenye Wilaya ya Tunduru kwa kuleta fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa,Zahanati,Miradi ya maji na Umeme wa REA.Pia Mwenyekiti alimpongeza Mbunge wa Tunduru Kusini Daim Iddy Mpakate kwa kazi kubwa anayofanya kusukuma spidi ya maendeleo kwenye jimbo hilo na hasa uwazi anaouweka kwenye matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo na namna anavyojitoa kusaidia wananchi wa jimbo hilo.
Post A Comment: