Taasisi ya Uhasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) imeendelea kutekeleza kikamilifu Vigezo vya Kimataifa vya EITI na Sheria ya TEITA ya mwaka 2015.


Hayo yamebainishwa na Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka TEITI Bw. Erick Ketagory katika maonesho ya kwanza ya Jukwaa la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini yanayoendelea Jijini Mwanza.  


Aidha, Ketagory ameeleza kuwa, tangu Tanzania imejiunga katika Asasi ya Kimataifa ya EITI imetoa ripoti zake kumi na moja (11) kuanzia Juni 2008 hadi Julai 2019 na ripoti ya 12  ipo katika hatua za mwisho  kukamilika na itawekwa wazi kabla ya mwezi Juni, 2022. 


Pamoja na mambo mengine, Ketagory amewaomba washiriki wa Jukwaa hilo kujenga tabia ya kusoma ripoti za TEITI ambazo zimesheheni taarifa mbalimbali kuhusu Sekta ya Uziduaji. 


Sambamba na hayo, Ketagory ameeleza kuwa,  ripoti za TEITI zinapatika kupitia mfumo wa kieletroniki wa dashboard unaopatikana katika tovuti ya TEITI ambayo ni www.teiti.go.tz.

Share To:

Post A Comment: