******************

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa mafunzo kwa wajasiriamali,Wazalishaji na wafungashaji wa bidhaa ya mchele katika Mkoa wa Mara.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo leo Mei 23,2022 Katibu Tawala wa Wilaya Tarime Mhe John Marwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara amesema kuwa azma ya serikali ni kuhakikisha kuwa nchi inajitosheleza katika uzalishaji wa mchele ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha kuagiza mchele kutoka nje.

"Nchi yetu inategemewa sana na nchi za jirani katika zao la mchele kwani sisi ndio tunazalisha kwa wingi pamoja na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika biashara ya zao hili bado wanatutegemea kwa kiasi kikubwa ". Amesema

Amesema mafunzo hayo ni njia muafaka wa kuleta tija zaidi katika juhudi za kuliletea taifa maendeleo ya haraka kulingana na fursa zilizopo hasa kwenye sekta ya viwanda,kilimo, biashara , uvuvi na maeneo mengine mengi.

Pamoja na hayo ameishukuru TBS kwa maandalizi ya mafunzo hayo muhimu na kuomba mafunzo hayo kuwa endelevu kwa nchi nzima ili yaweze kuleta maendeleo makubwa kwa taifa.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: