Na John Walter-Babati

Mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sillo ameandika historia katika Siasa za Tanzania katika awamu hii ya sita ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kuwa Mbunge wa kwanza kuwasilisha Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha mwaka mmoja Oktoba 2020 hadi Novemba 2021 katika jimbo lake la Babati vijijini mkoani Manyara.

Taarifa hiyo ya utekelezaji wa ilani iliyochapishwa katika kitabu chenye kurasa 47, imekuwa na mvuto wa kipekee kwa kuwa imeelezea jiografia nzima ya halmashauri ya jimbo la Babati vijijini, shughuli za kiuchumi ndani ya jimbo.

Sillo ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo wa kuchaguliwa, kwa awamu ya kwanza, amedhihirisha sifa yake hiyo, baada ya kuwasilisha Taarifa ya Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi hicho katika Mkutano wa wajumbe wa Halmashauri uliofanyika Jumanne Mei 31, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliopo Mjini Babati.

Aidha taarifa hiyo  imeainisha vipaumbele vya kimaendeleo pamoja na miradi ya kimkakati pamoja na fedha za mfuko wa jimbo zilizopokelewa kwa mwaka 2020/2021 jumla ya shilingi milioni 70,170,000 ambazo ziligawanywa katika kata zote 25 za jimbo hilo kulingana na maombi yaliyotumwa kwenye ofisi ya mbunge.


Share To:

Post A Comment: