Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila leo amewaapisha Viongozi  wa Serikali ya Wanafunzi (MASO) na amewataka viongozi hao kuwa mfano wa kuigwa katika matendo yao katika kipindi chote watakapokuwa chuoni.


Viongozi walioapishwa ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi Mohamed Hamad Hassan na Makamu wa Rais Grace Katabarwa ambao wote kwa pamoja  wametakiwa kufuata na kuzingatia miongozo, haki na wajibu pamoja na kumtanguliza Mungu katika utendaji wa majukumu yao.


Kwa upade wake Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia Taaluma Prof. Richard Kangarawe amewataka wanafunzi kuzingatia zaidi masomo na kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kuwa hilo ndiyo jukumu lao kubwa liliwapeleka Chuoni.


 Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi aliyemaliza   muda wake Godson Peter ameishukuru Menejimenti ya Chuo kwa malezi na mafundisho mema ambayo ameyapata yeye binafsi pamoja na viongozi wenzake huku akiahidi kuwa watakuwa mabalozi wazuri wa Chuo.


Share To:

JUSLINE

Post A Comment: