Julieth Ngarabali, Pwani


Watoto 200,967 wenye umri chini ya miaka mitano wanatarajiwa kupata chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa Polio mkoani Pwani kampeni itakayofanyika kuanzia Mei 18 hadi 21 mwaka huu katika vituo vya mbalimbali vya Afya, shule na nyumba kwa nyumba.


 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizindua kampeni hiyo Mei 18 mjini Kibaha amesema ugonjwa wa Polio ni hatari kwa sababu mtoto akiupata inaharibu kesho yake na pia anakua changamoto kwa familia yenyewe kwa sababu anakua anaishi na ulemavu usio na tiba miaka yote 


Kunenge ametoa rai kwa wazazi wote, viongozi wa dini, wa kimila , vyama vya siasa na watendaji kwa Serikali kuhakikisha wanawaelimisha na kuwahimiza wananchi kupata chanjo hiyo muhimu kwa maisha ya watoto kwa sababu haina madhara yeyote.


Awali Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Gunini Kamba amesema chanjo itatolewa kwa siku tatu na lengo la kufika kwenye maeneo yote ikiwemo nyumba kwa nyumba .


"Madhara ya ugonjwa wa Polio ni ulemavu wa ghafla wa viungo na usiotibika kwa hiyo ni muhimu sana kila mzazi na mlezi wawatoe watoto wapate chanjo hii ni salama , pia shughuli za ufuatiliaji na utoaji wa taarif za wagonjwa wanaopata ulemavu wa ghafla zitafanyika"amesema Dk. Kamba


Kwa upande wao baadhi ya wazazi akiwemo Elizabeth Mbega na Shanni Hassan wameshukuru Serikali kusogeza huduma hiyo hadi nyumbani kwa sababu chanjo itaweza kuwafikia hata wale watoto wanaoishi na walezi wenye umri mkubwa (wazee).


Tanzania imeamua kufanya kampeni nchi nzima baada ya Serikali ya Malawi kutoa tamko  Februari mwaka huu la kuwepo mlipuko wa Polio katika nchi hiyo baada mtoto mmoja kudhibitika kuwa na Polio na ni mara ya kwanza kwa bara ya Afrika kutokea kisa hicho baada ya kupita miaka mitano bila kisa cha ugonjwa huo.


Pia  ni sehemu ya utekelezaji Programu Jumuishi ya Taifa ya malezi . makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ,( PJT _ MMMAM ) 2022/2025 -26 inayolenga kujibu changamoto za mahitaji kwa watoto ili kuwekeza kwenye maendeleo ya ukuaji timilifu kwa mtoto.


Mwisho

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: