Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul sambamba na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini  Mhe. Tulia Ackson pamoja na  Wabunge na viongozi mbalimbali, wameshiriki mbio za kilomita tano katika  kilele cha mashindano ya riadha ya Mbeya Tulia Marathon yaliyofanyika leo tarehe 7 Mei, 2022 jijini Mbeya.

Mashindano hayo yaliyoanza tarehe 06 Mei, 2022 yamevutia wanariadha wengi kutoka ndani na nje ya nchi ambapo wamechuana katika mbio za  Kilomita 10, 21 na 42.

Share To:

Post A Comment: