Na John Walter-Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere amekabidhi kikombe Cha na cheti Kampuni ya Mati Super Brands Ltd inayozalisha pombe Kali kwa kuwa mshindi katika Sherehe za Mei Mosi zilizofanyika uwanja wa Kwaraa mjini Babati.

Wameshinda katika vipengele vya Banda Bora na kwenye maandamano.

Zawadi hizo zimepokelewa na mkurugenzi wa Kampuni hiyo David Mulokozi.


Mbali na Mati Super Brand Ltd, wengine waliokabidhiwa zawadi ni Chuo Cha ufundi stadi Manyara (VETA) na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (BAWASA).

Share To:

Post A Comment: