WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Innocent Bashungwa,akizungumza wakati akifungua  kikao cha jukwaa la maendeleo ya sekta ya fedha 2022 lililofanyika leo Mei 20,2022 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis,,akielezea jinsi Rais Samia anavyowajali wamachinga wakati wa  kikao cha jukwaa la maendeleo ya sekta ya fedha 2022 lililofanyika leo Mei 20,2022 jijini Dodoma.

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Lawrence Mafuru,akizungumza wakati wa kikao cha jukwaa la maendeleo ya sekta ya fedha 2022 kilichofanyika leo Mei 20,2022 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Taifa Bw. Ernest Masanja,akiipongeza Serikali kwa kuendelea kuwajali wamachinga nchini wakati wa kikao cha jukwaa la maendeleo ya sekta ya fedha 2022 kilichofanyika leo Mei 20,2022 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe,akizungumza wakati wa kikao cha jukwaa la maendeleo ya sekta ya fedha 2022 kilichofanyika leo Mei 20,2022 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula,akizungumza wakati wa kikao cha jukwaa la maendeleo ya sekta ya fedha 2022 kilichofanyika leo Mei 20,2022 jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ,akiwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika jiji hilo wakati wa kikao cha jukwaa la maendeleo ya sekta ya fedha 2022 kilichofanyika leo Mei 20,2022 jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi ,akizungumza wakati wa kikao cha jukwaa la maendeleo ya sekta ya fedha 2022 kilichofanyika leo Mei 20,2022 jijini Dodoma.

    

SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kikao cha jukwaa la maendeleo ya sekta ya fedha 2022kilichofanyika  leo Mei 20,2022 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Innocent Bashungwa,akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa mbalimbali mara baada ya kufungua  kikao cha jukwaa la maendeleo ya sekta ya fedha 2022 lkilichofanyika leo Mei 20,2022 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Innocent Bashungwa,akiwa katika picha na baadhi ya washiriki wa  kikao cha jukwaa la maendeleo ya sekta ya fedha 2022 lililofanyika leo Mei 20,2022 jijini Dodoma.

 

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Innocent Bashungwa, amewaagiza makatibu wakuu wa wizara za kisekta kukutana na kujadili fursa na changamoto zinazo wakabili machinga nchini ili serikali izifanyie kazi.

Waziri Bashunga,ametoa maagizo hayo leo Mei 20,2022 jijini Dodima wakati  akifungua kikao cha jukwaa la maendeleo ya sekta ya fedha 2022.

Aidha Kikao hicho kimetumika kujadili na kuweka mikakati ya serikali kuliwezesha kundi la machinga nchini.

Amesema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejikita katika kuliwezesha kundi la machinga kwa kuboresha na kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara.

Bashumgwa amesema kuwa mara baada ya kikao hicho kuisha makatibu wakuu wa wizara za kisekta wanatakiwa kukutana haraka ili kujadili changamoto na fursa zilizopo kwa machinga.

“Baada ya kikao hichi natoa maagizo kwa makatibu wakuu wa wizara za kisekta sisi Tamisemi,wizara ya fedha na mipango Maendeleo ya jamii, kukutana haraka ili kujadili changamoto zilizopo na fursa ili serikali iweze kuzifanyia kazi.

“Lakini pia mtafute mapendekezo na kuja na majibu yatakayo jibu changamoto za kundi hili pia kuona ni vitu gani ambavyo vinaweza kukwamisha mikakati na jitihada za serikali inayofanywa na serikali”amesema  Bashungwa

Waziri Bashungwa amesema kuwa serikali kupitia wizara ya Fedha na Mipango ipo katika mazungumzo na serikali ya India ili kupata mkopo wa masharti nafuu utakao tumika kuwezesha machinga.

“Tunafanya mazungumzo kupitia wizara yetu ya fedha na mipango kupata mkopo wa dola za kimarekani milioni 30 ambazo zitatumika kuwezesha machinga nchini”amesema

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis,amemshukuru Rais Samia kwa namna ambavyo anaendelea kuliinua kiuchumi kundi hilo.

“Rais ameelekeza vipaumbele katika sekta za uzalishaji kwenye kilimo,uvuvi na mifugo,nishati na kundi la machinga”amesema

Aidha amesema  kuwa kutokana na umuhimu huo Serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa kundi la Wamachinga linahudumiwa kwa upekee kwa kuratibu shughuli wanazozifanya ili ziweze kuwanufaisha na kuwaletea maendeleo.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Lawrence Mafuru, amesema kuwa Wizara yake ipo katika hatua za kutengeneza Bajeti Kuu ya Serikali, alisema miongoni mwa vipaumbele katika bajeti hiyo ambavyo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan angependa kuviona ni pamoja na sekta ambazo zinazalisha kama Kilimo, mifugo, uvuvi na nishati lakini pia wamachinga.

Amesema kuwa warsha ya wamachinga itasaidia kutoa fursa ya kujifunza lakini pia kuwa na sera itakayoelekeza rasilimali fedha kutoka kwa wadau mbalimbali inapatikanaje kwa ajili ya eneo hilo.

Mwenyekiti wa shirikisho la machinga nchini (SHIUMA) Ernest Masanja,ameipongeza  serikali kwa namna ambavyo inaweka mazingira rafiki kwa wamachinga.

Share To:

Post A Comment: