SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amemwomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kusimamia vyema matumizi ya fedha za Serikali kwa upande wa magari ya Serikali.Ametoa maelekezo hayo kwa Waziri Mkuu na kusema magari yote ya viongozi wa serikali yawe yanazimwa na dereva kushuka mara tu anaposhuka kwenye gari kiongozi huyo ili kupunguza matumizi mabaya ya mafuta.Dk.Tulia alitoa kauli hiyo jana Bungeni baada ya kumalizika kwa kipindi cha Maswali na majibu na baada ya kumaliza kuwatambulisha wageni waliokuja kulitembelea Bunge Jijini Hapa.Spika Dk.Tulia alisema kuwa kuna jambo ambalo linaonekana kuwa kero kwa kusababisha matumizi makubwa ya fedha za serikali hasa kwenye upande wa gharama kubwa za mafuta hususani magari ya viongozi.Kutokana na hali hiyo alisema kuwa hapo baadhi ya magari ya viongozi,kama vile mawaziri,manaibu mawaziri au makatibu  yanaposhusha viongozi yanaendelea kuwaka bila kuzimwa na bila kuzingatia kiongozi huyo atatumia muda gani kwenye shughuli zake.Kutokana na hali hiyo viongozi watakapokuwa wanashuka kwenye magari magari hayo yawe yanazimwa na dereva atoke kwenye gari na akae nje."Haiwezekani kiongozi anaposhusha gari linaendelea kuwashwa hadi saa mbili au tatu na dereva yupo ndani ya gari kusema kweli hiyo inasababisha gharama kubwa ya matumizi mabaya ya mafuta;"Fikiria hata sisi magari yetu binafsi tunapokumbana na foleni tunazima magari yetu sasa hii tabia ya kuwasha magari kwa muda mrefu bila kujua kiongozi atatoka saa nhapi hiyo siyo sahihi." Japo najua wapo viongozi ambao magari yao yanastahili kuwaka muda wote lakini wwngine waliobaki hapana tusifanye hivyo na hiyo haijalishi huko Bungeni au nje ya bunge popote magari ya viongozi yawe yanazimwa ili kupunguza gharama za matumizi ya fedha za mafuta"alielekeza Spika Dk.Tulia.Mwisho.

Share To:

Post A Comment: