MRADI mpya wa kimkakati wa Daraja jipya la WAMI ,limefikia asilimia 91 ikiwa Ni Pamoja na upande wa barabara unganishi ambayo imefikia asilimia 79.5.


Aidha Ujenzi wa mradi wa Daraja Hilo la kisasa unaendelea kwa Kasi kubwa na unatarajiwa kuanza kazi Julai mwaka huu.

Akifanya ziara ya miradi ya kimkakati ,kuona ujenzi ulipofikia Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, alisema Serikali ya awamu ya sita ,chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ,inaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ambayo yote ipo kwenye hatua nzuri.

Hata hivyo, alieleza , mradi huu ni tunu ya mkoa na Taifa na utagharimu zaidi ya sh.bilioni 75.134 bila VAT .

Kunenge alifafanua kwamba, daraja la WAMI la zamani lilijengwa 1959 na ni kiungo kutoka Chalinze kwenda mikoa ya Kaskazini mwa nchi yetu na nchi jirani.

"Daraja hilo halikidhi mahitaji ya magari yanayopita kwa kuwa lilijengwa miaka mingi iliyopita na ni jembamba lenye njia moja, barabara zinazounganisha daraja hili ziko kwenye miinuko mikali na kona mbaya ambapo ajali mbaya na vifo vimekuwa vikitokea mara kwa mara ,"

"Hili jipya likikamilika litakuwa Mkombozi ,kubwa urefu wa mita 510 na upana wa mita 11.85 linajengwa umbali wa mita 670 pembeni mwa daraja la zamani ."alisema Kunenge.

Alisema ,baada ya mkandarasi kukamilisha ujenzi huo atafanya ukarabati wa Daraja la zamani.

Kunenge alisema kwamba,Rais Samia aliahidi kufungua nchi kiuchumi na kumaliza utekelezaji wa ujenzi wa miradi iliyoanzishwa kipindi cha nyuma .

Vilevile Kunenge alipitia Mradi mwingine wa barabara ya Kwala -Vigwaza ni barabara ya wilaya yenye urefu wa kilometa 15.5 inayounganisha barabara Kuu ya Morogoro kupita katika vijiji vya Vigwaza, Mnindi na Kwala ambayo kwa Sasa inajengwa kwa kiwango cha Zege ili kurahishisha shughuli za uchukuzi kati ya bandari na barabara Kuu ya Morogoro.

Awali akimwakilisha meneja wa Wakala wa barabara ( TANROADS )Pwani ,Evelyn Mlai alisema ,ujenzi wa barabara unganishi utakamilika Novemba mwaka huu ,Ni barabara yenye urefu wa km.3.8 kwa kiwango cha lami yenye njia mbili zenye Jumla ya upana wa mita 12,ambapo mita 3.5 kwa kila njia yapitayo magari ,mita 2 za bega la lami na mita 0.5 za bega lisilo la lami kila upande.

"Kampuni inayosimamia kazi za ujenzi ni ILSHIN Engineers,& consultant co.ltd toka Jamhuri ya Korea Kusini ikishirikiana na Advanced Engineering Solutions Limited ya Tanzania kwa gharama ya sh.bilioni 6.3 bila VAT."alisema Evelyn.

Evelyn alieleza ,mkandarasi alianza kazi oktoba 22 mwaka 2018 Hadi sasa utekelezaji wa kazi umefikia asilimia 79.5.:;"Lakini katika daraja sehemu ya chini ya Daraja upo kwa asilimia 100 ikiwemo misingi na nguzo nne na kuta mbili za mwanzo na mwisho wa Daraja.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallah alibainisha ,daraja hili litakuwa na uwezo mkubwa katika usafirishaji na kufungua milango ya kimaendeleo na kukuza uchumi wa nchi yetu.

Aliwaambia Wana Bagamoyo Mradi ukikamilika wautumie kama fursa kwao ili kujiongezea tija.


Share To:

Post A Comment: