Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb)amewaasa wanafunzi wa kike kusoma kwa bidii ili waweze kuwa viongozi bora kwa Taifa.


Naibu Waziri huyo, ameyasema hayo leo, April Mosi,2022, kwenye Mahafali ya Kwanza ya kidato cha sita  Sekondari ya wasichana ya Bunge, ambapo Mhe, Mahundi alikuwa akimuwakilisha Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Aksoni.


Amesema, Taifa sasa chini ya Rais mama Samiah, limeweza kufikia asilimia ya 50 kwa 50 ya uongozi kwa wanawake, hivyo wanafunzi hao hawapaswi kukata tamaa.


"Rais Samia Suluhu Hassan, anaiongoza nchi tena kwa  uadilifu mkubwa, yupo Spika mwanamke, baraza la mawaziri na wabunge wengi ni wanawake na wanafanya kazi nzuri hiyo iwe chachu"alisema Mahundi.


Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: