WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya Mawaziri sita wa kisekta wakiongozwa na Waziri huyo pamoja na viongozi wa mkoa wa Tanga kulia  ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah UlegaWAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaz Dkt Angelina Mabula akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya Mawaziri sita wa kisekta wakiongozwa na Waziri huyo pamoja na viongozi wa mkoa wa Tanga
Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.Allan Kijazi akizungumza wakati wa kikao hicho
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa kikao hicho
MBUNGE wa JImbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula akifuatilia kikao hicho


 NA OSCAR ASSENGA, TANGA

WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angelina Mabula amewatahadharisha wananchi wenye tabia za kuvamia maeneo na kutegemea kwamba serikali itaridhia waendelee kuwepo jambo hilo halitajirudia tena.

Dkt Mabula aliyasema hayo leo mjini Tanga mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati ya Mawaziri sita wa kisekta wakiongozwa na Waziri huyo pamoja na viongozi wa mkoa wa Tanga.

Alisema ziara yao ni ya kwenda mkoa kwa mkoa kushughulia suala migogoro ya ardhi kwenye Vijiji 975 ambavyo baraza la mawaziri limeridhia viende kufanyiwa marekebisho au vingine kuondoshwa na vingine vifanyiwe mpango wa matumizi kutokana na maamuzi yatakayotoka

Alisema wakishafanya hivyo hawatarajii kuona kutakuwa na maeneo ya urasimishaji au kuridhia kumegwa maeneo watahitaji kila mmoja aweze kutekeleza wajibu wake kwa kutii sheria bila shurui maana hawawezi kuwa na mazoezi kama hayo kila mwaka

Alisema kwamba wameongea na viongozi wa mkoa wa Tanga hasa maadhimio waliyokubalina na baraza la mawaziri na Rais ameridhia waanze kupita kwenye mikoa ili waweze kutoa taarifa hizo ili mikoa wahusika na utekelezaji wake yaliyoamuliwa na serikali.

Waziri huyo alisema kwa mkoa wa Tanga kuna vijiji 18 kati ya vijiji 975 ambapo kati ya vijiji hivyo vijiji 14 kuna marekebisho kadhaa yatafanyika ,vijiji 4 kulingana na hali halisi wanaiona mustakabali wa nchi kama wataviachi viendelee kuwepo athari zake zitakuwa ni kubwa zaidi wanakwenda kufanya tathimini kuweza kujua hatma ya vijiji hivyo baada ya wao kuondoka wataacha timu mkoani Tanga.

Alisema timu hiyo itapita kwenye maeneo hayo wakifanya tathimini na mwisho wa siku watapeleka ushauri kwa serikali hatua za kuchukua lakini pamoja na tathimini mkoa kama mkoa watajipanga kwa ajili ya utekelezaji.

“Leo ilikuwa ni kuwapa maamuzi ya baraza la mawaziri ambayo yana baraka za Rais Samia Suluhu kwa hiyo suala la utekelezaji wanaanzia wapo ni jukumu la mkoa na timu yake,ushirikishwaji katika suala zima la utekelezaji maamuzi hayo ili isitokee mtu akalalamikia kuonea au kufanyaje jukumu lao kama serikali ni kuhakikisha wanatoa elimu ili masuala hayo yasijirudie”Alisema

Alisema kwa sababu wamekuwa na operesheni mbalimnbali mwisho wa siku usimamizi wake unakuwa sio mzuri matokeo yake yanajirudia kipindi hiki chini ya Rais Samia Suluhu angependa kuona mambo hayo yanajirudia na ndio maana kwenye wizara ya ardhi ameridhia kutoa fedha nyingi ili waweze kumalizikana na migogoro ya watumiaji ardhi.

Waziri huyo alisema hivyo wanalolifanya ni mendelezo kuona kila mmoja awajibike ndio maana alisisitiza Mkuu wa mkoa ,Wilaya,Maafisa Tarafa na watendaji chini kila mmoja akisisimie jukumu lake suala kama hilo halitaweza kujirudia tena,

“Lakini nitoe rai kwa wananchi watakaokuwa wametengewa maeneo na  kuweka mpango bora wa matumizi ya ardhi hatutarajii kuona mnaingi maeneo ya hifadhi yaliyozuiliwa ,mnaingiakwenye maeneo ya vyanzo vya maji,maeneo ya taasisi mbalimbali ambazo wamekuwa wakivamia maana hayo ndio yametufikisha hapa tulipo”Alisema Waziri Dkt Mabula

Hata hivyo alisema kila mmoja watumishi wa serikali na watendaji wanayo nafasi yao katika kufanya usimamizi mambo hayo yasijirudii ikiwemo wananchi watii sheria bila shurti.

“Lakini niwaambie kwamba kwamba kwa wale ambao wanavamia maeneo na kutegemea serikali itaridhia waendelee kuwepo pale hilo halitajirudi tena tukishafanya maamuzi hatutarajii kuona kutakuwa na maeneo ya urasimishaji au kuridhia kumega maeneo”Alisema Waziri Dkt Mabula.

Awali akizungumza wakati wa kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alianza kwa kumpongeza Waziri Dkt Mabula huku akieleza mkoa wa Tanga wameshaanza kupambana na migogoro ya ardhi kutokana na uwepo wa ushirikiano mzuri baina yao na Kamishna wa Ardhi na watu wake wanawasaidia sana.

Alisema siri moja wanawasaidia kwa sababu wanapokwenda kwake anawaambie wasimumunye maneno kwani wao sio wanasiasa,wao wakija waniambia jambo hili lipoje historia yake na kuna maeneo mengine kuna onekana kuna siasa na kuna maeneo maamuzi yanaonekana ni eneo la siasa.

Mkuu huyo wa mkoa alisema  lakini ikienda unakuta kuna vijiji vimeanzishwa na serikali imepeleka huduma za muda mrefu ikiwemo shule za Msingi,Hospitali hivyo wanapokwenda kuwaambia maeneo yao sio rasmi wanaanzisha mgogoro na kuwatia watu wasiwasi.

“Lakini hayo ndio umekuja na kamati kuyaondoa na hayo ni mambo makubwa yaliyofanywa na kamati na ni mafanikio..Tanga na kuna maeneo ya muheza ya Mkonge yaliyokuwa rasmi ya serikali watu wamevamia na katika kuvamia wenye umiliki hawakukemea jambo hilo miaka sita au tano iliyopita  sasa wanakuja kufata matumizi yake ya maeneo yao”Alisema

Aidha alitolea mfano eneo la uwanja wa ndege kuna watu wameingia kuna mipaka na kuna watu wameingia na kutaka kuipeleka serikali mahakamani na sasa hawana ndege kubwa kutokana na uwepo wa mgogoro na wananchi.

“Sasa tumewaachia miaka 10 serikali nimeambiwa mtaingia kwenye ukarabati  wanatafakari tunaomba huo mgogoro umalizike mapema ili mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege uendelee na kufungua fursa”Alisema

Naye kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Dkt Allan Kijazi alisema kamati hiyo imepita maeneo mbalimbali na kuweza kutoa mrejesho wa maamuzi ya baraza la mawaziri kuhusu migogoro iliyopo kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Alisema baada ya kutolewa maamuzi hayo ilikubaliana kamati hiyo ya mawaziri nane ipite nchi nzima kueleza nini kimeamuliwa kwa migogoro hiyo ambayo ipo muda mrefu na imekuwa ni kero kwa wananchi.

Mwisho.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: