Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof.Stephen Maluka akitembelea mabanda ya wadau wa utafiti kutoka maeneo mbalimbali nchini wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam. Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof.Stephen Maluka akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uvumbuzi DUCE, Prof.Amani Lusekelo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam. Makamu Rasi,Taaluma,Utafiti na Huduma kwa jamii DUCE, Dkt.Christina Isingo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam.Mtoa Mada Mkuu Prof. Nuhu Hatibu akiwasilisha mada katika uzinduzi wa Wiki ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam. Mtoa Mada Bw. Yahya Mgawe akiwasilisha mada katika uzinduzi wa Wiki ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Msaidizi (Mipango, Fedha na Utawala)Dkt. Method Samwel akizungumza katika uzinduzi wa Wiki ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam. Mtoa Mada Dkt.Katherine Fulgence akiwasilisha mada katika uzinduzi wa Wiki ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam.Meza Kuu ikiongozwa na Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.Stephen Maluka wakisimama kwaajili ya wimbo wa Taifa katika uzinduzi wa Wiki ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa Sekondari Chang'ombe wakiimba wimbo wa Taifa katika uzinduzi wa Wiki ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam. Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.Stephen Maluka akipata picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa utafiti wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam.

***************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kimewataka watafiti wa masuala mbalimbali kutumia tafiti zao kutatua changamoto zilizopo katika jamii pamoja na kuzilinda tafiti hizo ili ziweze kuleta manufaa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha DUCE Prof Stephen Maluka wakati wa uzinduzi wa Wiki ya 7 ya Tafiti na Uvumbuzi Aprili 20-22 iliyozinduliwa leo Katika Viwanja cha Chuo hicho Jijini Dar es Salaam.

Wiki ya utafiti na uvumbuzi inafanyika kwa mara saba ambapo ilianzishwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 2015 baada ya kuona umuhimu wa tafiti zinazofanywa na wanataaluma, wanafunzi wa shahada ya kwanza na ya pili kuleta tija kwa jamii.

Prof Maluka amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa wiki ya utafiti na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ilikua ni kuhakikisha tafiti zinazofanywa na wanataaluma na wanafunzi zinasaidia jamii na sio kuishia katika Majarida na vitabu.

“Wiki hii ya utafiti tunataka kuona tafiti zinaoneshwa na wanataaluma hawa zinaenda kuleta tija kwa jamii, na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kiliamua kuanzisha wiki hii mwaka 2015 baada ya kuona tafiti nyingi zinafanyika ila zimekuwa zinaisha kwenye majarida na vitabu na kutokusaidia jamii,”amesema Prof Maluka

“Kwa mwaka huu sisi kama DUCE tunaahidi kuzisaidia tafiti zinazofanywa kuingia katika soko la bidhaa pamoja na kuzilinda tafiti hizi ili zisiibiwe na watu wengi na kutumika,”

Aidha, Prof Maluka amewataka wanataaluma hususani wanafunzi kujifunza mambo mazuri yanayofanywa na watafiti wa Chuo hicho na kuweza kupata mawazo ya tafiti watakazokuja kuzifanya.

Ameongeza kuwa, katika wiki hii ya tafiti kutafuta na ushindani na washindi watakaofanya vizuri watapata nafasi y kushiriki Wiki ya tafiti Chuo Kikuu cha UDSM.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Lugha Prof Amani Msokelo amesema jumla ya watafiti 54 wamejitolea kuonesha tafiti zao kwa mwaka 2022 huku asilimia 85 ni wanataluma na asilimia 15 ni wanafunzi kutoka shule za Mazoezi za Chang’ombe.

Amesema kwa mwaka huu kauli mbiu ya Wiki ya Tatifi ni Tafiti na Uvumbuzi wenye Tija na chuo cha Duce kimeingia makubaliano na Vyuo kutoka Marekani na Denmark kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali.

Chuo cha Duce kimewataka wadau wengine wa maendeleo wa sekta ya elimu kuendelea kushiriki na kutoa mchango wao katika Wiki ya Utafiti na Uvumbuzi.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: