Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dk Jonathan Budenu.


 Raisa Said,Tanga


Mkoa wa Tanga unatarajia kutoa chanjo ya ugonjwa wa polio Kwa watoto zaidi ya laki tatu walio chini ya umri wa miaka mitano kuanzia April 28 hadi Mei 3 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa mkoa ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa wakati wa kikao cha kamati ya afya ya msingi ngazi ya mkoa (PHC) ambacho kimefanyika Leo.

Amesema kuwa ni muhimu watoto wote ambao wamelengwa kufikiwa katika zoezi hilo wakaweza kupatiwa chanjo hiyo Ili kuwakinga na madhara ya ugonjwa huo.

"Nendeni mkazishirikishe kamati za afya ngazi ya jamii Ili waweze kutoa uwelewa Kwa wananchi kuhusu chanjo hiyo Ili pale zoezi litakapoanza walengwa wote waweze kufikiwa Kwa wakati"amesema Kaimu RC huyo.

Aidha aliwataka wataalamu wa Afya kwenda kutoa elimu sahihi juu ya madhara ya ugonjwa wa polio Ili wazazi waweze kuwatayari kuwachanja watoto hao wakati wa zoezi hilo.

Amesema kuwa iwapo wazazi au walezi wataweza kupata taarifa sahihi kuhusu chanjo hiyo itarahisisha wananchi kujitokeza Kwa wingi wakati wa utoaji wa chanjo na hivyo kufikia lengo Kwa haraka.

"Niwaombe Kila mmoja Kwa nafasi yake tusaidiane kutekeleza jukumu hili kwani wakati tuliona na ni mdogo na nimuhimu kuwafikia watoto wote hata wale ambao wameruka chanjo na ambao tayari walishapata hapo awali Ili wote waweze kupatiwa chanjo hii"alisisitiza DC Mgandilwa

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Dk Jonathan Budenu amesema kuwa matumizi sahihi ya vyoo ndio kinga dhidi ya usambazwaji wa ugonjwa huo.

"Ugonjwa huu unaambukizwa Kwa njia ya chakula na wadudu wanashambulia mfumo wa chakula hivyo ugonjwa huu Hauna kinga ni vema watoto wakapatiwa chanjo ili kuwakinga na madhara ya viungo kupooza"alisema Dk Budenu.

Aidha amesema kuwa tayari mkoa umeshaanza kuchukuwa tahadhari zote hususani katika maeneo ya mipakani Kwa kuhakikisha wageni wote wanaoingia nchini wanapatiwa chanjo ili kujihakikishia usalama wao.

Hata hivyo Programu za malezi jumuishi nchini Tanzania zinahitaji kupewa kipaumbele na msisitizo kutokana na kukosekana kwa uratibu mzuri na zinatekelezwa kama sehemu za programu za kisekta au tafiti zinazofanywa na wadau zikilenga baadhi ya umri wa watoto na kutekelezwa kwenye maeneo machache Kutokana na umuhimu wa Mfumo wa Malezi Jumuishi,.

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa MMMAM imeandaa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto itakayo tekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (2021/22-2025/26).

Mpango huu umelenga kutatua changamoto za ukuaji na maendeleo ya watoto wenye umri wa miaka 0-8. Programu hii itatoa mchango katika kufanikisha Mpango wa tatu wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano.

Share To:

Post A Comment: