Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewataka wanafunzi wa Shule ya Msingi Zamzam iliyopo Dodoma Jiji kumtanguliza Mungu na kuweka jitihada katika masomo yao ili kuweza kufikia mafanikio ya kitaaluma na kidini na hivyo kutoa mchango wao katika ujenzi na ustawi wa Taifa Tanzania.


Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa  hafla ya futari kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Zamzam ya Jijini Dodoma, hafla ambayo amekuwa akiwaandalia wanafunzi hao kila mwaka wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,katika shule hiyo asilimia kubwa ya wanafunzi ni watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.


Katika hafla hiyo ambayo aliongozana na Uongozi wa BAKWATA mkoa,Viongozi wa CCM Kata na Timu ya DODOMA JIJI,Mbunge Mavunde ameahidi kuchangia kilo 1000(tani moja) ya mchele,mafuta ya kula lita 300 jezi za watoto wa kiume na kike,pamoja na magoli ya Chuma kwa ajili ya uwanja wa Michezo uliopo shuleni.


Wakisoma Risala yao kwa Mbunge Mavunde,wanafunzi hao wameshukuru Mbunge Mavunde kwa moyo wake wa kuwajali kila mwaka kwa kushiriki nao futari na kumuomba aendelee kuwa nguzo katika kuwasaidia watoto wanaosoma Zamzam ili waweze kufikia malengo yao ya kimasomo.

Share To:

Post A Comment: