Mwandishi wetu   Kibaha.   


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu  Hassan anatarajiwa kushiriki kwenye mdahalo wa kuadhimisha kumbukizi ya kitaifa ya miaka 100 ya  kuzaliwa kwa muasisi wa Taifa  Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


Mdahalo huo unatarajiwa kufanyika Aprili 09 katika chuo cha Uongozi cha mwalimu Nyerere  kilichoko Kibaha mkoani Pwani. 


Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Pwani Mkuu wa mkoa huo Abubakari Kunenge amesema mdahalo huo umeandaliwa na Chama cha Mapinduzi na una lengo la kutafakuri maisha ya Mwalimu Nyerere .


"Mwaka huu ikifika Aprili 13 nchi yetu itakua ikiadhimisha kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na sisi Pwani tutaadhimisha sambamba na kufanyika madahalo mkubwa ulioandaliwa na CCM na utawahusisha watu mbalimbali wa kada tofauti tofauti na bila kujali itikadi za kisiasa"amesema Kunenge na kuongeza


"Mdahalo utafanyika Jumamosi Aprili 09 kwenye chuo hicho  na kwa mujbu wa taarifa nilizonazo Rais Samia atakua mgeni rasmi  hivyo nawakaribisha wananchi wote wa Pwani na Tanzania nzima kushiriki katika tukio hili muhimu  linaloanza saa mbili asubuhi na kwamba viwanja vitakua tayari kupokea watu  kuanzia saa saa 12 asubuhi siku hiyo "


Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani amemshukuru Rais Samia kwa kuupa heshima  kwa mara ingine tena katika Mkoa huo na pia ameishukuru CCM kwa kuandaa tukio hilo mkoani humo..


Kunenge ameongeza kuwa jambo muhimu ni kwamba Hayati Baba wa Taifa ni kiongozi wa wote  na hivyo ni vema kila mtu akashiriki kwenye kumbukizi hiyo


Mmoja wa wakazi wa Kibaha Bella Johson amesema uamuzi wa CCM kufanyia mdahalo huo kwenye chuo hicho ni mzuri na ni mfano wa kuigwa katika miaka ijao kwa sababu moja ya sababu ya kuanzishwa kwake ni kuenzi fikra za Hayati Mwalimu Nyeree kwa vitendo।.


Hayati Baba wa Taifa  alizaliwa April 13 , mwaka 1922  kijijini Butiahama mkoa wa Mara na alifariki  Oktoba 14  mwaka 1999.Share To:

JUSLINE

Post A Comment: