Teddy KilangaArusha.Mwekezaji mzawa wa kiwanda cha maziwa(New Northen) na mjasiriamali wa mazao mbalimbali,John Kyenkungu arejea kumiliki mali yake aliyokuwa amenyang'anywa na mtu asiyefahamika tangu mwaka 2019
Mali hiyo ni Kiwanda alichonunua sh.milioni 440 serikalini mnamo mwaka 1999 ambacho kipo katika kiwanja namba 4-13 kitalu D katika kata y Ungalimited jijini Arusha kwa lengo la kuwekeza ili kujiinua kiuchumi na kusaidia watanzania kupata ajira.
Akizungumza mbele ya vyombo vya habari mbalimbali,Mwekezaji huyo,Kyenkungu alisema kiwanda kilikuwa kina uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita 60 za maziwa ambapo kupitia uwekezaji wake aliweza kuajiri watu zaidi ya 100 wakiwemo vijana.
Kyenkungu alisema kiwanda hicho kilichokuwa tegemezi katika maisha yake ambapo aliweza fikia hatua ya kukodisha mashamba ya West Kilimanjaro lengo likiwa ni kupanua biashara yake ya maziwa kwa kuweza kuzalisha kwa wingi maziwa katika kiwanda chake pamoja na kusaidia wakulima na wafugaji kupata faida kupitia biashara wanazofanya.
"Wakati naendelea kujihimarisha zaidi kwenye kiwanda changu ghafla nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa anatoka Ofisi ya Msajili wa hazina ambaye alinitaka nifikie Arusha ikiwa mimi nilikuwa Dar es Salaam lakini baadaye nilifika katika eneo langu la kiwanda,"alisema Mwekezaji huyo.
Alisema baada ya yeye kuwasili  mkoani Arusha katika eneo lake la biashara walijitokeza kundi la watu wanaokadiliwa ishirini ambao hawafahamu na hawakujitambulisha mahali walipotoka wakampatia barua iliyoonyesha notisi kwa stakeholder meeting.
"Barua hii ilikuwa ni confidential iliyoandikwa mei 27,2019 ambapo ilionyesha imetoka Ofisi ya Msajili wa hazina ambapo ilisainia na Peter Gwalilo lakini aliyeileta sikumtambua kutokana na kutojitambulisha,"alisema.
Kyenkungu alisema baada ya hapo aliona kikundi cha watu kikiongozana na polisi waliokuwa na bunduki wakimwambie achague mawili kati ya kupewa kesi ya uhujumu uchumi au aachie kiwanda hicho ambapo walidai kuwa kinarudishwa kwa serikali yeye alijibu ni vyema wakamfunga lakini hawakufanya hivyo.
"Baada ya hapo nilirudi Dar es Salam kutokana na ndipo nilipokuwa nafanya shughuli zangu ndogo ndogo lakini waliwaondoa wapangaji wangu katika magodauni yangu pamoja na walinzi wakawaweka wa kwao,"alisema.
Hata hivyo alisema baada ya kufika Dar es Salaam alifika na kutafuta njia nyingine ya kuishi kutokana na hali ya msongo wa mawazo aliyokuwa nayo katika kipindi hicho cha kunyang'anywa mali yake aliyokuwa anahitegemea na alishindwa kuwekeza chochote katika kiwanda hicho tangu alipoporwa mali hiyo na mtu asiyejulikana.
"Katika maisha yangu sikutegemea kama kuna kitu kama hicho kinaweza kutokea katika maisha yangu lakini baada ya mwaka mmoja nikapigiwa simu na watu ambao hawakujitambulisha kunataka nifike benki kuu ambapo nilipofika niliwakuta watu kama 20 kwenye chumba na walisema hawawezi kujitambulisha kwangu,"alisema Muwekezaji huyo.
Aliongeza kuwa katika kikao hicho kilichofanyika BOT alienda na Mwanasheria wangu na Consultant laki waliwakataa na kudai wanamuhitaji yeye tu na baada ya kubaki walimsisitiza kuwa akitaka uzee wake uende salama ni vyema akarudisha hati ya kiwanda kile serikalini la sivyo watampeleka uhujumu uchumi.
"Nilichosema kwani niko tayari na wala sikutaka kupoteza muda mwingi ikiwa kipindi hicho nipo na msongo wa mawazo ambapo niliona ni bora niende uhujumu uchumi tu nikiona hata nilipokuwepo nilikuwa sina namna ya kuishi,"alisema.
Naye wakili Emmanuel Antony alisema mteja wake hadi sasa ni mmiliki halali wa kiwanda hicho hivyo hana budi kurejea kwenye mali yake kutokana alinunua kihalali kwani kitendo cha kuchukuliwa na mtu asiyejulikana ni mazingira ambayo hayana baraka za serikali.
"Kitendo hicho hakina baraka kwa serikali kutokana na kuwa na taarifa zote za ununuzi wa kiwanda hicho lakini pamoja na hilo watu waliokuwa wanakuja kiwandani hawakujitambulisha kwa mmiliki wa kiwanda,"alisema Wakili huyo.
Pia alisema barua yenyewe ya notisi aliyoletewa imeandikwa ni ya siri  ambayo ilikuwa wito wa kikao cha wadau na mawasiliano yenyewe yaliyokuwa yanafanyika baina ya mteja wake na hao watu wasiojulikana yalikuwa ya siri hivyo kupitia vigezo hivyo ni dhahiri kuwa hiyo siyo serikali bali ni mtu asiyejulikana ambaye ni mpokonyaji wa mali hiyo na sasa anayohaki wa kurudi katika mali yake.

Share To:

Post A Comment: