Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa komputa mpakato kwa Maafisa Elimu Kata 26 wa Halmashauri ya wilaya ya Meru ambapo amewataka Maafisa elimu hao kutunza na kutumia komputa hizo kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.
Makwinya amesema hayo wakati wa hafla ndogo ya kukabidhi laptop hizo kwa waratibu ambapo, pia ametoa wito kwa wadau kuwezesha upatikanaji wa chaji za nishati ya jua (solar)kwenye shule ambazo hazina nishati ya umeme .
Akitoa taarifa ya Komputa hizo Mwl. Marcus Nazi ambaye ni Mkuu wa Idara ya Elimu Awali na Msingi amesema Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kupitia mradi wa LANES II, imetoa komputa 26 kwa Maafisa Elimu kata 26 za Halmashauri hiyo ambayo ni miongoni mwa Halmashauri 20 zilizonufaika na komputa kati ya Halmasauri 185 za Tanzania bara.
Kwa upande wake Mhe.Jeremia Kishili M/Kiti wa Halmashauri ya wilaya ya Meru ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita kwa kutoa vitendea kazi hivyo,pia kumekuwa na mwamko mkubwa wa shughuli za Maendeleo ndani ya Halmashauri .
Afisa Elimu Kata,Kata ya Shambarai Burka mwl. Regina Lekule kwa niaba ya Maafisa Elimu Kata wengine ameishukuru Serikali kwa kuwapa komputa hizo kwani awali ilikuwa ni changamoto kubwa katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa kwa wakati na kwa usahihi .
Ikumbukwe .Halmashauri ya Wilaya ya Meru inakata 26 zenye shule za Msingi 180,kati ya Shule hizo shule 116 ni shule za Serikali na Shule 64 ni shule binafsi.
Post A Comment: