Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali imepanga kuajiri watumishi 32,000 katika sekta mbalimbali zenye uhaba wa watumishi.


Hayo ameyasema leo Aprili 06, 2022 Bungeni wakati akijibu maswali ya wabunge juu ya Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuajiri watumishi wapya hasa katika Sekta ambazo hazina utoshelevu wa watumishi.


“Mheshimiwa Rais na Serikali yake wametambua tatizo hili la uhaba wa Watumishi na hasa kwenye miradi Ya Sekta ya Afya na Sekta ya Elimu na hivyo basi Mheshimiwa Rais ametoa kibali, ahadi ya serikali kwa mwaka huu wa fedha tulikuwa tuajiri watumishi 44,000 tayari Serikali ilishaajiri watumishi wapya na watumishi wa Ajira mbadala 12,000.


“Ninaomba niwathibitishie Waheshimiwa wabunge, Mheshimiwa Rais ameridhia wiki ijayo nitatoa tangazo rasmi la ajira 32,000 na utaratibu wa ajira hizo na mgawanyo wake katika Sekta ambazo zinaongoza kwa uhaba wa watumishi maelezo yote nitayatoa wiki ijayo,” Mhe. Mhagama.

Share To:

Post A Comment: