Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi Dk.Angelina Mabula na Mkurugenzi wa Shirika la Koica kutoka Korea ambalo limefadhili mchakato wa kurasimilisha ardhi kimila kwa Halmashauri ya Ikungi Kyucheol Eo (katikati) wakimkabidhi kitabu cha mpango wa matumizi bora ya  Ardhi ya Kijiji cha Mnang'ana Mwenyekiti wa kijiji hicho Pascal Mdini katika hafla ya utoaji hati miliki za kimila kwa baadhi  ya wananchi iliyofanyika wilayani Ikungi mkoani Singida juzi.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi Dk.Angelina Mabula (wa pili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Wananchi wa Vijiji vya  Ntondo na Nkwea baada ya wajumbe hao kuwakabidhi hati zao za kimila katika hafla iliyofanyika kwenye vijiji hivyo  vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida juzi.
Mjumbe wa kamati hiyo Hawa Mwaifunga akimkabidhi hati Mkazi wa Kijiji cha Nkwea Iddi Tibaijuka.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi Dk.Angelina Mabula na Mkurugenzi wa Shirika la Koica kutoka Korea ambalo limefadhili mchakato wa kurasimilisha ardhi kimila kwa Halmashauri ya Ikungi Kyucheol Eo (katikati) wakimkabidhi hati ya Ardhi ya Kijiji cha Mnang'ana Diwani wa Kata ya Sepuka Halima Ng'ula.
Mkuu  wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge akizungumza katika hafla hiyo katika Kijiji cha Nkwae.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi akitoa taarifa ya mpango wa matumizi bora ya ardhi katika wilaya hiyo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi akizungumza katikahafla hiyo.
Meneja Mradi kutoka UN Women Lilian Mwandanga akitoa taarifa ya shughuli wanazozifanya katika wilaya hiyo.
Wakuu wa Idara balimbali wa Mkoa wa Singida wakiwa kwenye hafla hiyo Kushoto ni Kamishna wa Ardhi MsaidiziMkoa waSingida Shamimu Hozza,
Mmoja wa Wakazi wa Kijiji cha Nkwae aliyepata mafunzo ya matumizi bora ya ardhi akielezea mpango huo mbele ya Wajumbe Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi Dk.Angelina Mabula, viongozi na wananchi.
Mjumbe wa kamati hiyo Jafari Wambura Chege akizungumza baada ya kutolewa kwa taarifa ya mpango bora wa matumizi ya ardhi mkoaniSingida.
Mjumbe wa kamati hiyo  Soud Mohamed Jumah  akizungumza baada ya kutolewa kwa taarifa ya mpango bora wa matumizi ya ardhi mkoaniSingida.
Mmoja wa Wakazi wa Kijiji cha Nkwae aliyepata mafunzo ya matumizi bora ya ardhi akielezea mpango huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC Eliya Digha akizungumza katika hafla hiyo.
Wananchi wa Kijiji cha Nkwae wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mjumbe wa kamati hiyo , Asia Halamga akizungumza kwenye hafla hiyo. Kushoto ni     Mjumbe wa Kamati hiyo Dk. Florence Samizi.
Mjumbe wa kamati hiyo, Jeseph Kamonga akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Nkwae katika  hafla hiyo. 
Mwenyekiti wa kamati hiyo Ally Makoa akimkabidhi hati mkazi wa Kijijicha Nkwae Asha Swalehe.
Mjumbe wa Kamati hiyo Dk. Florence Samizi akimkabidhi hati mkazi wa Kijijicha Nkwae Majaliwa Shabani.
Mjumbe wa kamati hiyo , Asia Halamga akimkabidhi hati Mkazi wa Kijiji cha Nkwae Benjamini Shija.
Wananchi wa Kijiji cha Nkwae waliokabidhiwa hati zao wakiziangalia.
Wananchi wa Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa hati hizo.
Baadhi ya madiwani wa Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakikabidhiwa hati.

 


Na Dotto Mwaibale, Singida


WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi Dk.Angelina Mabula ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kufanikisha Mpango wa Matumizi ya Ardhi pamoja na upimaji ardhi wilayani humo.

Dk.Mabula alitoa pongezi hizo katika hafla ya utoaji hati miliki za kimila kwa baadhi  ya wananchi iliyofanyika wilayani Ikungi mkoani Singida juzi na kuhudhuriwa na mamia ya watu.

“Niipongeze halmashauri ya wilaya ya Ikungi kwa kufanikisha mpango huu wa kutoa hati miliki za kimila kwa wananchi ambapo leo tunashuhudia hati 5050 zikitolewa ili ni jambo zuri la kuigwa na halmashauri nyingine” alisema Mabula.

Aidha Dk. Mabula alishuhudia wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakitoa hati 54 kwa wananchi wa vijiji vya Ntondo na Nkwea vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida huku wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati  hiyo Ally Makoa.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa hati hizo Makoa alisema, kazi ya upangajii iliyofanywa na wizara ya ardhi kupitia mradi wa KKK unatimiza kiu na matarajio ya Wizara pamoja na ilani ya Chama cha Mapinduzi.

 Aidha, Kamati hiyo imempongeza pia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutolewa Sh.ilingi Bilioni 50 kwa ajili ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi unaotekelezwa katika halmashauri nchini. 

Halmashauri ya wilaya ya Singida ina jumla ya vijiji 84 kati ya vijiji hivyo vijiji 20 vinapitiwa na Mkuza wa Bomba la Mafuta na Mipango ya Matumizi bora ya ardhi imeandaliwa katika vijiji 16 kati ya 20 na kufanya jumla ya vijiji 50 katika wilaya ya Singisa kuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeitaka Wizara ya Ardhi kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikishajj ardhi kwenye maeneo mbalimbali ili kufikia mwaka 2025 iwe imetimiza malengo na matakwa ya Wizara na kuboresha sekta ya ardhi ili kuiwezesha serikali kuinua uchumi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ikungi Justice Kijazi akisoma taarifa ya mradi wa urasimishaji na umilikishaji wa ardhi kimila alisema takribani hati 5050 za zimemilikishwa kwa wananchi huku wanawake wakimili hati 2030 sawa na asilimia 40.2 lakini imani potofu ya kumnyima mwanamke kumiliki ardhi ikiwa ni moja ya changamoto katika halmashauri hiyo. 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge alisema kitendo cha kupima na kurasimisha ardhi kinafungua fursa za uwekezaji ndani ya mkoa huo kwa kuwa thamani ya ardhi inaongezeka baada ya kurasimishwa huku Mkurugenzi wa Shirika la Koica kutoka Korea ambalo limefadhili mchakato wa kurasimilisha ardhi kimila kwa Halmashauri ya Ikungi Kyucheol Eo alisema shirika hilo linashirikiana na serikali katika kuleta usawa kati ya mwanamke na mwanaume ikiwemo katika umiliki na matumizi bora ya ardhi. 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: