Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akimuonesha  kitu Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini  (TARURA ) Wilaya ya Ikungi, Mhandisi Ally Mimbi (kushoto) wakati wa kamati hiyo ilipokuwa ikikagua moja  ya madaraja katika barabara ya Utaho Makiungu wilayani humo jana.
Meneja wa Wakala wa Usambajzaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini na Mijini (RUWASA) Wilaya ya Ikungi, Mhandisi Hopeness Liundi (kushoto) akitoa taarifa  ya utekelezaji wa maji wa Ikungi kwa kamati hiyo.
Ukaguzi wa tenki la maji la mradi wa Ihanja ukifanyika .
Ukaguzi wa ujenzi wa tenki la maji la mradi huo ukifanyika.


Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Oliva Njoka akitoa taarifa ya ujenzi wa miundombinu ya Hospitali hiyo mbele ya kamati hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi (kushoto) akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa hospital hiyo.
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Hospitali hiyo.

Msimamizi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi cha VETA, John Thomas (kushoto) akielezea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
Mwenyekiti wakamati hiyo Mika Likapakapa akienda kukagua moja ya jengo la Chuo cha Ufundi VETA.
Ukaguzi wa Karakana ya kutengenezea magari mradi wa Chuo cha VETA ukifanyika 
Mafundi wakiendelea na kazi
Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini  (TARURA ) Wilaya ya Ikungi, Mhandisi Ally Mimbi (kushoto)  akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Utaho-Makiungu. 
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa kwenye ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo.
Mjumbe wa Kamati hiyo Ally Mwanga (katikati) akitoa maelezo kwa wajumbe wakati wa ukaguzi wa moja ya daraja lililopo katika barabara hiyo ya Utaho-Maiungu.
Ukaguzi wa madaraja ukiendelea.
Ukaguzi wa ujenzi wa madaraja ukiendelea.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mandimu Abdallah Ramadhani akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa darasa.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mika Likapakapa akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
Wajumbewa kamati hiyo wakitoka kukagua mradi wa darasa katika shule hiyo.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Abubakar Muna akizungumza wakati kamati hiyo ilipokuwa ikikagua ujenzi wa mradi wa Kituo cha Afya cha Kinyampembee.
Mjumbe wa Kamati hiyo Ally Mwanga ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kinyampembee. Wengine kutoka kushoto ni wajumbe wa kamati hiyo, Stamili Dendegu, Martha Andrew na   Jafari Dude.
Wajumbe wa Kamati hiyo na wananchi wakikagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kinyampembee.
 


Na Dotto Mwaibale, Singida.KAMATI  ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi mkoani  Singida imekagua miradi 11 ya maendeleo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya hiyo na  kuridhishwa na matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wake.

Akizungumza kwa nyakati tofauti juzi na jana wakati kamati hiyo ikikagua miradi hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Mwenyekiti wa chama hicho wilayani humo Mika Likapakapa  alisema ameridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo katika halmashauri hiyo licha ya kuwepo kwa changamoto ndogondogo.

"Kwa kweli tunawapongeza kwa kuitendea haki miradi hii ambayo Serikali inatumia fedha nyingi kuitekeleza hivyo nawaombeni kuendelea kutumia nguvu hiyo hiyo ya  ushirikiano ya kufanya kazi hii ya kutekeleza miradi yetu yote kwenye wilaya yetu," alisema Likapakapa.

Likapakapa alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo na kuwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kuitunza kutokana na umuhimu wake.

Alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kutoa fedha za miradi na ni wajibu wa wananchi nao kuhamasika kuunga jitihada za serikali kwa kujitolea kufanya kazi zingine za maendeleo ambazo zipo ndani ya uwezo wao.

Likapakapa aliwaomba wahandisi wa wilaya hiyo kujenga tabiaya kutembelea mara kwa mara na kukagua miradi inayojengwe ili ikamilike kwa wakati.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ally Mwanga aliwataka wakandarasi waliopewa kutekeleza miradi kuikamilisha kwa wakati kabla walivyo saini kwenye mikataba yao na si vinginevyo.

“Tunawaomba wakandarasi mliyopewa kazi ya kujenga miradi hii jengeni ndani ya muda mliokubaliana katika mkataba na kazi hiyo iwe ya viwango kulingana na thamani ya fedha mliyopewa” alisema Mwanga.

Wajumbe wa kamati hiyo wakizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo waliwapongeza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Justice Kijazi, Mkuu wa Wilaya Jerry Muro, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Ally Mwanga pamoja na wakuu wa idara na viongozi mbalimbali kwa kusimamia utekelezaji wa  miradi hiyo kwa uaminifu

Baadhi ya  miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo ni utekelezaji wa mradi wa maji Ikungi ambao gharama yake ni Sh.313,718,795.75,  Utekelezaji wa mradi wa Maji Kata ya Ihanja wenye thamani ya Sh. 368,813,749.50, Ujenzi wa Miundombinu ya Hospitali ya Wilaya ya Ikungi ambao ulitengewa kiasi cha Sh.1,500,000,000, Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu Shule ya Msingi Mandimu iliyopo Tarafa ya Mungaa ambaouligharimu Sh. 20 Milioni.

Miradi mingine iliyokaguliwa na kamati hiyo ni Utekelezaji wa miradi ya barabara za Utaho-Makiungu na Siuyu- Nali na Makotea ambao utagharimu jumla Sh.488,301,400.00, Mradi wa Ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA, Kituo cha Afya cha Kata ya Kinyampembee na Ntuntu pamoja na Mradi wa Umeme wa Kata ya Makiungu ambao utazinufaisha kaya 50.

Leo  Kamati ya siasa ya Mkoa wa Singida itafanya ziara ya namna hiyo katika Halmashauri za Wilaya ya Ikungu na kukagua miradi iliyopo  Kata ya Irisya.

Ziara hiyo ya kamati ya siasa  iliwahusisha viongozi na wataalamu mbalimbali wa wilaya hiyo ikiongonzwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Mika Likapakapa pamoja na Katibu wa CCM wa wilaya Stamili Dendegu.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: