Kituo cha Afya Zayu kilichopo Kata ya Bagamoyo Katika Halmashauri ya Korogwe Mkoani Tanga(Picha zote na Yusuph Mussa)
Mwanamke Amina Kea wa Kijiji cha Mkata Magharibi Kata ya Mkata Tarafa ya Mazingara wilayani Handeni akifurahia baada ya kujifungua mtoto wa kiume February 26,2022 na kupewa jina la Abdulrahman"Putin" katika Kituo cha Afya Zayu  kilichopo Kata ya Bagamoyo  katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe mkoani Tanga Barabara Kuu ya Korogwe -Handeni (Picha na Yusuph Mussa)
Muuguzi wa Kituo cha Afya Zayu Kilichopo Kata ya Bagamoyo katika Halamshauri ya Mji wa Korogwe barabara kuu ya Korogwe-Handeni Hilda Singano akimpima uzito mtoto wa miezi sita (Picha na Yusuph Mussa)
MKURUGENZI Mtendaji Msaidizi wa Kituo cha Afya Zayu Kilichopo Kata ya Bagamoyo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mkoani Tanga Barabara kuu ya Korogwe-Handeni Jamilah Masoud akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo na mipango ya kituo hicho(Picha na Yusuph Mussa)
Mtaalamu wa Maabara kituo cha Afya Zayu Kilichopo Kata ya Bagamoyo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe barabara kuu ya Korogwe-Handeni Peter Msuva akiwa kazini(Yusuph Mussa)
Kituo cha Afya Zayu kilichopo Kata ya Bagamoyo katika Halamshauri ya Mji wa Korogwe barabara kuu ya Korogwe-Handeni kulia ni Jengo la Utawala,vyumba vya madaktari,wodi za kawaida na huduma nyengine na kushoto ni wodi ya VIP (Yusuph Mussa)
GARI la kubabea wagonjwa kituo cha Afya Zayu kilichopo Kata ya Bagamoyo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mkoani Tanga (Picha na Yusuph Mussa)

NA YUSUPH MUSSA,KOROGWE
 
WANANCHI  zaidi ya 500 katika Halmashauri ya Mji Korogwe mkoani Tanga wamefaidika na upimaji wa bure wa afya zao kwenye zoezi lililofanywa na Kituo cha Afya cha Zayu kilichopo Kata ya Bagamoyo mjini Korogwe.


Katika zoezi hilo, wananchi saba walikutwa na ugonjwa wa ngirimaji (busha), watatu walikuwa na ugonjwa wa henia na mmoja kidole tumbo, na wote walifanyiwa upasuaji papo hapo. Lakini wanawake sita walikutwa na dalili za saratani ya shingo ya kizazi.


Hayo yalisemwa  (Feb. 28) na Shara Harith ambaye ni Tabibu wa Kituo cha Afya Zayu, na kuongeza kuwa katika upimaji huo, wanawake wawili walikutwa na viashiria vya saratani ya shingo ya kizazi.


"Baada ya kuona wananchi hawana utamaduni wa kupima afya zao mpaka waumwe, kituo chetu kina utaratibu wa kupima afya bure kwa wananchi ambao wengi wao wanapata huduma kwetu. Katika zoezi hili tumeweza kupima wananchi 340, ambapo kati yao, saba walikutwa na ngirimaji, watatu walikuwa na henia, mmoja kidole tumbo na wanawake wawili walikutwa na viashiria vya saratani ya shingo ya kizazi" alisema Harith.


Harith alisema zoezi kama hilo pia walilifanya Septemba, 2020, ambapo zoezi hilo lililenga kuwapima wanawake saratani ya shingo ya kizazi, ambapo wanawake 255 walijitokeza, na kati yao sita walikutwa na dalili za saratani hiyo, na waliweza kuwasaidia kwa kuwasafirisha bure kwa gari la wagonjwa wa kituo hicho kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bombo, Tanga.


"Tunapofanya mazoezi haya ya upimaji, tunawashirikisha madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Magunga. Tunawapima afya yao, na tunapowakuta na kesi mbalimbali, wengine tunawafanyia upasuaji hapa hapa kwenye kituo chetu cha afya kwa kiwango kidogo cha fedha, na wale wenye changamoto kubwa, tunawasafirisha kwa gharama zetu kwa kutumia gari letu la wagonjwa kwenda Hospitali ya Bombo" alisema Harith.


Harith alisema ujio wa Bima ya Afya ya NHIF Septemba, mwaka jana, imeongeza nguvu katika utoaji huduma kwenye kituo hicho cha afya, kwani pamoja na huduma nzuri waliyokuwa wanatoa kwa jamii, Bima ya Afya ilikuwa kikwazo, kwani baadhi ya watumishi wa Serikali, Sekta Binafsi na mtu mmoja mmoja ambao walikuwa na bima hiyo, walishindwa kupata huduma kwenye kituo hicho cha afya.


"Tumeanza kutoa huduma kupitia Bima ya Afya ya NHIF Septemba, mwaka 2021. Na hiyo itarahisisha utoaji huduma kwa watumishi wa Serikali, Sekta Binafsi na baadhi ya makundi yanayotumia bima kwenye jamii. Malengo yetu ni kusogeza huduma kwa wananchi ikiwa ni pamoja na mazoezi ya upimaji afya kwa wananchi mara kwa mara ili kuwaibua watu wenye shida mbalimbali kupata tiba kwa wakati, kusaidiana na Serikali kutoa huduma za afya, na kuongeza majengo mengine ya wodi za wagonjwa" alisema Harith.


Naye Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi wa Kituo cha Afya cha Zayu, Jamilah Masoud, alisema wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwani imetoa wigo mpana kwa taasisi binafsi ikiwemo Sekta ya Afya kuchangia kutoa huduma kwa wananchi, na ndiyo maana na wao wamevutiwa kusaidia jamii kwa kufanya zoezi la upimaji afya bure.


"Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha kuunga mkono Sekta Binafsi katika kufanya shughuli za kuhudumia jamii pamoja ikiwemo Sekta ya Afya. Sisi tumekuwa tukiendesha mazoezi ya kuwapima afya bure wananchi, na wale wanaokutwa na matatizo, tunawafanyia upasuaji kwa gharama nafuu. Lakini na wale wanaohitaji rufaa, tunawapeleka kwa gharama zetu kwa kutumia gari la Kituo cha Afya Zayu" alisema Masoud.


MWISHO.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: