Na mwandishi wetu,Kilimanjaro

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kigaigai Leo ametembelea eneo la mradi wa kufua umeme wa Kikuletwa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro na kutoa maagizo mbambali juu ya utekelezaji wa mradi huo.Miongini mwa maagizo hayo ni pamoja na kuwataka watekelezaji wa mradi huo ambao ni chuo cha ufundi Arusha(ATC) kutafuta hatimiliki ya eneo la mradi huo lenye jumla ya ekari 354 haraka iwezekanavyo.

Kigaigai ametoa muda wa miezi mitatu kwa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Hai na halmashauri ya Hai kuhakikisha wanakamilisha mchakato wa hatimiliki ya eneo lote la mradi ili kuepuka wavamizi.

“Chuo cha Ufundi fuatilieni mpate hatimiliki yenu haraka iwezekanavyo ili muweze kulilinda eneo hili lisivamiwe na wavamizi” alisema Kigaigai

Mbali na kutoa maagizo hayo Kigaigai aliwahakikishia usalama watekekezaji wa mradi huo kwa muda wote huku akisisitiza kwamba eneo hilo la mradi kwa sasa ni eneo la kimkakati na serikali italilinda muda wote.

Mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji wa mradi huo,Dkt Eric Mgaya alisema jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,37 bilioni zinataraji kutumika kugharamia mradi wa kufua umeme wa Kikuletwa uliopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Alisema Fedha hizo zimetolewa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka benki ya dunia ambapo zinataraji kugharamia mradi huo unaotaraji kuleta tija na mapinduzi katika sekta ya nishati ya umeme hapa nchini.

Alisisitiza kuwa mradi huo unataraji kuzalisha wataalamu wa masuala ya umeme ambao watatumika katika mradi wa maji wa bwawa la Mwalimu Julius Nyerere uliopo mkoani Pwani.

Dkt Mgaya alisema kwamba mradi huo umeshaanza kutekelezwa na mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu ramani ya mchoro wa mradj wote itakuwa imeshakamilika.

Naye mkuu wa chuo cha ufundi cha Arusha(ATC),Dk Musa Chacha alisema kwamba lengo kuu la chuo chao kutekeleza mradi huo ni kuzalisha wataalamu ambao watakwenda kufanya kazi katika bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere.

Dkt,Chacha alisema kwamba tayari wameshaanza kutekeleza mradi huo kwa kukarabati make to ya zamani ndani ya kituo hicho na kuajiri watumishi mbalimbali.

Kituo cha kufua umeme cha Kikuletwa kilianzishwa miaka ya 1930 na wakoloni wa Kijerumani ambapo kilikuwa kikizalisha umeme kwenye gridi ya taifa kwa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo Chuo Cha Ufundi Arusha (ATC) walikabidhiwa na serikali mwaka 2013 kwa malengo ya kukiendeleza

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: