Wanafunzi wa Kitanzania wa TEHAMA kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma waliibuka miongoni mwa wanafunzi bora zaidi katika shindano la TEHAMA Huawei 2021-2022 Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Likiwa na kaulimbiu ya “Connection, Glory, Future”, shindano hilo lilihitimshwa tarehe 19 Februari, huku zaidi ya nchi 15 na timu 38 zikifanya mitihani ya maandishi na maabara. Shindano hili lilivutia zaidi ya washiriki 15,000 kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Shindano la TEHAMA Huawei 2021-2022 Kusini mwa Jangwa la Sahara lilizinduliwa katika kanda ya Afrika miaka sita tu iliyopita, limekua na kuwa shindano kubwa zaidi la ujuzi wa TEHAMA barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Tanzania iliwakilishwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma na kila timu ilikuwa na wanafunzi . Timu za Tanzania zilijishindia zawadi ya kwanza (Cloud Track), zawadi ya pili, na zawadi ya Tatu (Network Track).

Wanafunzi hao ni Mafiu Khatibu, Daniel Mathew na Ndabuye Sengayo (UDOM), James Mushi, Erick Shemdoe, na Zuwena Hamoud (UDSM) na Joan Makyao, Kivuyo Kelvin, na Peter Edward (UDSM). Timu zote tatu zimeingia Fainali za Dunia zitakazofanyika nchini China mwezi Mei ikitanguliwa na hafla ya Kukabidhi Tuzo itakayofanyika nchini Afrika Kusini Aprili mwaka huu.

Akizungumzia mafanikio hayo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Zanzibar Bwana Ali Khamis Ali alisema; “Kama nchi tunajivunia vijana hawa wenye vipaji kwa ushindi mkubwa walioupata katika Fainali za Kanda za Shindano la TEHAMA la Huawei, ushindi wao unathibitisha ubora wa kitaaluma wa Vyuo vyetu vya Elimu ya Juu, tunatumai na kuamini watang’ara na kuwa mabalozi wazuri wa Tanzania. katika duru ya kimataifa.

Naipongeza Huawei kwa mipango hii na tunatarajia kuona juhudi hizi zaidi na zaidi kwa mfumo wa ikolojia wa vipaji wa TEHAMA ulio imara na endelevu nchini."

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania, Tom Tao, aliwapongeza wanafunzi hao kwa ushindi wao mkubwa akisema; “Huawei Technologies itaendelea kushirikiana na serikali na Taasisi za Kitaaluma katika kutoa mafunzo ya TEHAMA kwa wanafunzi wa Kitanzania vijana na kuhakikisha kuwa maarifa na ujuzi wanaopata vijana hao ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa Tanzania kijamii na kiuchumi”

Zuwena Hamoud Salum, mmoja wa wanafunzi wawili wa kike wa kwanza kushinda Shindano la TEHAMA la Huawei aliwahimiza wanafunzi wa kike kushiriki katika Shindano hilo huku akitoa shukrani zake kwa nafasi ambayo Huawei wamewapatia.

“Nawaomba na kuwahimiza wanafunzi wenzangu wa kike kuchangamkia fursa hizi zinazotolewa na Huawei kupitia shindano la TEHAMA la Huawei. Jukwaa hilo litawawezesha kuonyesha utaalam wao wa TEHAMA na kuudhihirishia ulimwengu kuwa wanawake wanaweza na wako tayari kutoa mchango zaidi katika Sekta ya TEHAMA nchini na kimataifa kwa ujumla.

Kwa hivyo tuchukue nafasi kwa mikono yetu wenyewe na kuzichangamkia, tuwe na ujasiri na kujiamini, tunaweza kufanya kilicho bora zaidi." Alisema.

Shindano la TEHAMA Huawei 2021 lilijumuisha zaidi ya nchi 80 ulimwenguni, likiwa na washiriki 150,000 kutoka zaidi ya vyuo vikuu na vyuo vikuu 2,000. Shindano hilo lilizinduliwa katika kanda ya Afrika miaka sita tu iliyopita.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: