p>
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda akizungumza na Wananchi (hawapo pichani) wakati akitatua mgogoro wa barabara ya kutoka Mtekente kwenda Msansao na Ujungu uliotokana na baadhi ya wananchi kugomea isipite katika mashamba yao. Mgogoro huo aliutatua jana wakati Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo  zilipomaliza kukagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Tarafa ya Ndago wilayani humo mkoani Singida jana.
Wajumbe wa kamati hiyo hiyo wakikagua ujenzi wa darasa katika Shule ya Sekondari ya Ushora.
Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Ashery Samuel akizungumza na Wananchi wa Tarafa ya Ndago (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa matundu ya vyoo ya Kituo cha Afya cha Ndago.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza kwenye ziara hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba Pius Sangoma akizungumza na Wananchi wa Tarafa ya Ndago wakati wa mkutano huowa hadhara.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda akizungumza na Wanafunzi wa Sekondari ya Ushora wakati wa ziara hiyo.
Ukuguzi wa moja ya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Ushora ukifanyika.
Viongozi hao wakisaidia kubeba ndoo zenye zege wakati ujenzi wa Kituo cha Afya Mwanduigembe ukiendelea.
DC Mwenda akishiriki kubeba ndoo yenye zege wakati wa ujenzi wa kituo hicho. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo pamoja na wakuu wa idara wakiwa wamejipanga foleni wkwa ajili ya kusaidia kumwaga zege kwenye ujenzi wa kituo hicho cha fya.Afisa Elimu Msingi wa wilaya hiyo Asia Matitu akishiriki kubeba zege.
Mmoja wa mafundi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya akitoa maelezeo kwa wajumbe wa kamati hizo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba,Hussein Sepoko akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya.
Ukaguzi wa ujenzi wa Sekondari mpya ya Ndulungu ukiendelea.
Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Iramba Ezra Mwacha akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa maji wa Kata ya Kaselya.


Ukaguzi wa  ujenzi wa tenki la maji la Mradi wa Kaselya ukiendelea.Diwani wa Kata ya Kaselya Juma Ramadhani akiishukuru Serikali kwa kupeleka mradi huo wa maji katika kata hiyo.

Wananchi wa Tarafa ya Ndago wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.
Mkutano ukiendelea.
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Iramba, Michael Abas akichangia jambo kwenye mkutano wa hadhara wa Tarafa ya Ndago.


Na Dotto Mwaibale, Iramba


SHILINGI BILIONI 10 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan katika mwaka mmoja wa uongozi wake zimewezesha kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika Tarafa ya Ndago iliyopo Wilaya ya Iramba  mkoani Singida.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda  wakati akiwahutubia  Wananchi wa Tarafa ya Ndago kwenye mkutano wa hadhara baada ya  kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo  zilipomaliza kukagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Tarafa hiyo jana.

Mwenda alisema kamati hizo zilifanya ukaguzi wa miradi hiyo ili kuona nini kimefanyika katika mwaka mmoja wa uongozi wake Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ametoa fedha nyingi  kwa ajili ya kutekeleza miradi katika Tarafa hiyo.

Aliwataja alioongozana nao kufanya ukaguzi huo kuwa ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo na kamati ya siasa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo na timu yake wakiwemo wataalam, Mwenyekiti wa Halmashauri na kamati ya ulinzi na usalama.

Alisema mambo yaliyofanyika katika wilaya hiyo ni mengi na kuwa wamepanga kila Tarafa kati ya nne zilizopo waielezee miradi iliyofanyika ambapo wameanza na Tarafa ya Ndago yenye kata sita ambayo ni kubwa kuliko tarafa zingine zote katika wilaya hiyo ambapo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imetekelezwa miradi yenye thamani ya Sh. 10. Bilioni.

Alisema yeye kama kiongozi mkuu wa Serikali na CCM wameona baada ya kufanya ukaguzi huo waitishe mkutano  wa hadhara ili waweze kuwaeleza walichokiona katika miradi hiyo, changamoto zilizopo,inaendeleaje, usimamizi wake upoje, lini itakamilika na watarajie nini.

Alisema miradi ya elimu iliyotekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan katika shule za msingi wamekamilisha ujenzi wa  darasa moja Shule ya Msingi Senenkwa ambalo limegharimu Sh.11.3 Milioni, ujenzi wa darasa moja Shule ya Msingi Azimio ambapo pia wamepeleka kiasi hicho cha fedha.

Mwenda alisema wamekamilisha ujenzi wa bweni moja katika Shule ya Watoto wenye mahitaji maalumu ya Songambele ambapo wamepeleka Sh.80. Milioni, kumalizia chumba kimoja cha darasa Shule ya Sekondari Mtekente  walipeleka Sh.20 Milioni, ujenzi wa chumba kimoja cha darasa Shule ya Sekondari Ulugu  walitoa Sh.20 Milioni.

Aliongeza kuwa wamejenga vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Ushora ambapo pia walitoa Sh.40 Milioni, ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Ndulungu tayari tumetoa fedha awamu ya kwanza Sh.470 Milioni na awamu ya pili tunategemea kupokea Sh.130 Milioni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Alisema kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo ya Sekondari kutaifanya Tarafa nzima ya Ndago kila kata kuwa na shule ya sekondari hivyo ni jambo la kujivunia na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyowafanyia Wana Ndago.

Akizungumzia sekta ya Afya alisema wanajenga Kituo cha Afya Mwanduigembe ambapo Serikali itawapelekea Sh.500 Milioni, ujenzi wa Kituo cha Afya Ulugu kwa gharama ya Sh.500 Milioni tayari wamepokea Sh. 250 Milioni.

Mwenda alisema tangu nchi hii ipate Uhuru Tarafa ya Ndago ilikuwa na kituo kimoja tu cha afya na hicho kilichopo ambacho wanakitumia kilijengwa mwaka 1976 kikiwa ni Zahanati ndogo na ilikuwa kabla hata ya CCM hakijazaliwa lakini ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan anajenga vituo viwili vya afya katika kila kata ili ni jambo la kushangilia kwani ni zaidi ya miaka 50 kulikuwa na kituo hicho kimoja tu.

"Ni mwaka mmoja tu wa uongozi wake amefanya hivyo je akimalizia na hiyo miaka yake tisa kuwa madarakani si atajenga vituo vya afya katika kata zote za Wilaya ya Iramba" alisema Mwenda.

Akizungumzia Maji alisema katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan wamepelekewa Sh. 465 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji Zinziligi na Sh.730 Mradi wa Maji Kaselya yote ikiwa Tarafa ya Ndago.

Akizungumzia ujenzi wa barabara ya Malango alisema wamepeleka Sh.201 Milioni na sasa inafanya kazi, alisema wanafungua barabara kutoka Ulugu, Mang'ole hadi Mpugizi ya kilometa 9.5 kwa gharama ya Sh.765 Milioni.

Alisema wanajenga barabara ya ya kutoka Mtekente, Msansao hadi Ujungu ambapo wametoa Sh.999 Milioni karibu Bilioni moja na mkandarasi anaendelea na kazi, ujenzi wa barabara ya Kibaya, Luzurukulu hadi Kipuma ambayo inajengwa kwa Sh.624 Milioni.

"Hivi ndugu zangu kuna Rais kama Mama Samia ambaye ameweza kutoa hela nyingi kiasi hiki tena katika Tarafa ya Ndago tu na si Wilaya nzima ebu pigeni hesabu ninyi wenyewe" aliuliza Mwenda kwenye mkutano huo huku yakipigwa makofi kwa ajili ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Mwenda alisema mambo hayo ya maendeleleo hayajafanyika katika kata hiyo pekee bali ni kata zote za wilaya hiyo ya Iramba na kuwa hayo ni baadhi tu kwani hajazungumzia ujenzi wa madarasa ya UVIKO na umeme.

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba Ashery Samwel alisema wameridhishwa na matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo na aliwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kuitunza badala ya kuisubiri Serikali.

Alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kutoa fedha za miradi na ni wajibu wa wananchi nao kuhamasika kuunga jitihada za serikali kwa kujitolea kufanya kazi zingine za maendeleo ambazo zipo ndani ya uwezo wao.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Innocent Msengi alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za miradi katika wilaya hiyo ambapo aliwaomba wakandarasi kujenga miradi hiyo kwa viwango kulingana na fedha walizolipwa.

Aidha Msengi alitoa wito kwa wananchi wa wilaya hiyo kujenga tabia ya kulipa ushuru wa mazao ili kusaidia wilaya hiyo kukusanya mapato yatakayosaidia kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.

Diwani wa Kata ya Ndago Ernest Kadege alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Mbunge wao Dk. Mwigulu Nchemba kwa kufanikisha miradi hiyo katika Tarafa hiyo na jimbo zima la Iramba Magharibi.

Wajumbe wa kamati hiyo wakizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo waliwapongeza viongozi wote wa wilaya hiyo, wakuu wa idara kwa ushirikiano mkubwa walioutoa na kufanikisha miradi hiyo kutekelezwa miradi hiyo kwa uaminifu  kwa ufanisi mkubwa.wakuu wa shule na viongozi waliosimamia fedha za kutekeleza miradi hiyo kwa uaminifu na kuifanikisha.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda alifanikiwa kumaliza mgogoro wa barabara ya kutoka Mtekente kwenda Msansao na Ujungu uliotokana na baadhi ya wananchi kugomea isipite katika mashamba yao lakini baada ya kufanyika kwa mkutano wa hadhara uliongozwa na Mwenda wakiwepo viongozi mbalimbali wananchi hao waliridhia barabara hiyo ipite katika eneo hilo baada ya kuomba wiki moja ya kuondoa mazao yao katika maeneo itakapo pita barabara hiyo ambayo ni muhimu kwa maendeleo yao.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: