Na Mwandishi Wetu


Mtandao namba moja nchini Tanzania kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali Tigo , wameshirikiana na Kampuni ya Samsung kuwaletea Watanzania Toleo jipya la Simu la SAMSUNG S22. 


Akizungumza wakati wa kuitambulisha Samsung S22 Meneja wa Maduka na Bidhaa za Intaneti kutoka Tigo Tanzania Bwana Mkumbo Myonga amesema kuwa Kampuni ya Tigo inazidi kuwaletea Watanzania kilicho bora kuhakikisha wanaendelea kuishi maisha ya Kidigitali kwa kuwaletea simu Janja kali na za kisasa zaidi"Samsung S22 zinakuja na Ofa ya Intaneti ya GB 96 BURE Mwaka Mzima , kama mnavyoona simu hizi zina kioo kikubwa, na mwonekano wenye kuvutia kwahyo na matumizi yake ni makubwa pia , kwahiyo kama ilivyo kawaida yetu Tigo Tanzania tunawahakikishia Watanzania kuwa simu hizi ni bora sana zikiwa na Waranti Orijino kutoka Samsung ,  hasa katika Ulimwengu huu wa Kidigitali zaidi , ".

Kwa upande wake Meneja wa Samsung Tanzania Bwana Sulleiman Mohamed amesema kuwa 


" Tunafurahi sana kwa mara nyingine tena kuungana na Tigo katika toleo hili la Samsung S22 series ambapo Watanzania watafurahia simu zetu hasa kupitia Mtandao wa 4G Kutoka Tigo, maana huwa tunashirikiana na Kampuni Zenye huduma bora kama zilivyo simu zetu, simu hizi za Samsung S22 Series zinapatikana kuanzia leo Dunia nzima na kwa leo hakika tunawapongeza Tigo kwa kuwezesha watanzania waweke kufikiwa na Toleo hili mapema zaidi tena zikiwa na Ofa ya kurekebisha kioo BURE ndani ya mwaka mzima kama ikitokea kikavunjika na Waranti ya Miezi 24" Alisema Bwana Sulleiman


Simu za Samsung S22 Series zinapatikana kwenye maduka ya Tigo na Samsung nchi nzima kuanzia leo Machi 18, 2022.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: