MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ametembelea eneo linapojengwa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA),wilaya ya Ikungi na kufurahishwa na hatua inayoendelea kwa sasa.

Ujenzi huo ulianza mwaka 2019 baada ya serikali kukubali kutenga fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 2 ili kijengwe chuo cha kisasa cha ufundi chenye fani mbalimbali ikiwemo ufundi wa magari,umeme,kompyuta,ushonaji na ujenzi.

Akizungumza katika ziara hiyo Machi 7,2022,Mtaturu amesema awali Mkandarasi alipewa ujenzi huo na chuo cha Veta Tawi la Singida lakini ujenzi haukwenda vizuri hadi maamuzi ya wizara kuelekeza Mkurugenzi wa Veta Kanda ya Kati John Mwanja achukue jukumu la kuendeleza ujenzi huo.

“Leo ninayo furaha kutembelea ujenzi huu na kupewa maelezo ya kina na ndugu yangu Mwanja kuwa wameweka mkakati wa kuanza ujenzi wiki hii,”alisema.

Amesema kwa mujibu wa maelezo ya Mkurugenzi huyo ni kwamba mafundi watawekwa kila jengo na kufanya kazi usiku na mchana ili ifikapo Juni Mwaka huu wawe wamekamilisha tayari kuanza masomo.

Mtaturu amewaomba kuweka mkakati mzuri wa kukamilisha mapema ujenzi huo ili udahili wa wanafunzi ufanyike na masomo yaanze Mwaka huu.

#AwamuYaSitaKaziniSingidaMasharikiKaziIendelee #.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: