Na,Jusline Marco:Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Said Mtanda amelipongeza jiji la Arusha kwa kuwa miongoni mwa majiji yanayofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na kuwaletea wananchi maendeleo.

Ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mwaka mmoja ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika Wilaya ya Arusha ambapo amesema mafanikio yoyote ya kimaendeleo yanajengwa kutokana na fedha.

Mtanda amesema mafanikio hayo yametokana na ufuataji wa maelekezo ya serikali ambayo yalitaka ukusanyaji wa mapato utumie mifumo wa lipa upewe risiti hivyo kipelekea jiji la Arusha kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na kuimarisha vitendea kazi vya kukusanyia mapato.

Aidha amesema zaidi ya shilingi Milioni 49 imetumika kwa ajili ya kununua Post mashine 150 ikiwa ni katika juhudi za kuongeza tija,adhima na malengo ya serikali jiji la Arusha kutoka shiliningi bilioni 23 hadi kufikia shilingi bilioni 30 ifikapo mwaka 2022/2023 .

"Miongozo ya serikali inasema tunapokusanya mapato asilimia 40 iwe ya uendeshaji na asilimia 60 iwe kwa ajilibya miradi ya maendeleo ambapo jiji la Arusha tunayo miradi mikubwa na midogo ambayo tumeifanya."alisema Mtanda

"Tumeona namna ambavyo jiji la Arusha tumejikita katika kutengeneza shule za ghorofa na kila mwaka hadi sasa zaidi shule 6 za ghorofa zimejengwa ndani ya jiji la Arusha kutokana na mapato ya ndaji."aliongeza Mtanda

Mtanda amesema upande wa elimu msingi jiji la Arusha limeendelea kupokea fedha zaidi ya shilingi milioni 781 kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia kwa ajili ya elimu bure ambapo kwa upande wa elimu sekondari wamepokea fedha zaidi ya shilingi bilioni 1.03 kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu kupitia dhana ya elimu bila malipo katika jiji la Arusha ambapo fedha hiyo imefanya shughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyoo.

Vilevile amesema serikali ya wilaya itaendelea kusimamia Sekta ya elimu ambapo jiji la Arusha kwa miaka 5 mfululizo limekuwa namba moja katika ufaulu kwa elimu ya shule ya msingi na kwa upande wa elimu sekondari wamepokea zaidi ya shilingi milioni 690 ambazo zimetumika kujenga vyumba vya madarasa 105 kupitia program ya UVIKO 19.

"Nitumie fursa hii kuipongeza idara ya elimu sekondari kwa usimamizi wa mradi huo wa UVIKO 19 na mpaka sasa taarifa ambayo ninayo sisi ni miongoni mwa watu ambao tumefanya vizuri katika mradi wa UVIKO 19 ."alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Arusha mjini

Sambamba na hayo katika sekta ya Afya ,Mtanda amesema malengo ya serikali ya Wilaya ni kuifanya hospitali ya Wilaya ya Arusha kuwa hospitali ya kiutalii ambayo itawatibu hadi watalii wanaofika jiji la Arusha ambapo zaidi ya milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la OPD ma serikali kuu kuahidi kutoa shilingi bilioni 1 huku malengo yakiwa ni kutumia shilingi 1.5 pamoja na ujenzi wa kituo cha afya cha Mkonoo ulikigharimu shilingi milioni 550.

Ameongeza kuwa utoaji wa huduma katika afya umefikia asilimia 98 ikiwa ni upatikanaji na utoaji wa dawa muhimu zilizopo katika orodha ya serikali na vifaa tiba, zaidi ya shilingi milioni 336 zimetumika kwa ajili ya kununua madawa na vifaa tiba ambapo amesema kupitia mapato ya ndani ya bilioni 23 tayari zahanati 3 zimewezeshwa huku zaidi ya shilingi milioni 150 zikiwekezwa katika sekta ya afya ili kuboresha vituo vya afya na ujenzi wa nyumba za wataalam.

Pamoja na hayo Mtanda amesema katika bilioni hizo 23 zinazo kusanywa asilimia 10 itumike kwa ajili ya vijana ,wanawake na watu wenye ulemavu hivyo jiji la Arusha kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia,zaidi ya shilingi bilioni 3 zimeshatolewa ambazo zimetumika kukopesha makundi hayo huku wanawake wakitumia bilioni 1.1 kwa vikundi 251 kukopeshwa,vijana wakitumia shilingi bilioni 1.3 na vikundi 122 vikikopeshwa ,watu wenye ulemavu wakipewa shilingi milioni 124 na vikundi 123 vikikopeshwa.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa katika sekta ya umeme ambapo katika kipindi cha mwaka mmoja ndanibya jiji la Arusha wanamradi wa Periabani wenye thamani ya shilingi bilioni 4 uliolenga kuweka umeme kwenye kaya 1500 na tayari kaya 654 zimeshaunganishwa na huduma ya umeme hasa katika maeneo ambayo yameingia ndani ya jiji lakini yanaonekana ni vijiji miji ambapo TANESCO kipitia mapato yake ya ndani kwa jiji la Arusha wana mradi wa shilingi bilioni 3 na wateja elfu 25 kuunganishiwa umeme.

Katika sekta ya barabara Mkuu huyo wa Wilaya amesema barabara katika jiji la Arusha ni Kilometa 781 kati ya hizo kilometa 92 ni barabara za lami,kilometa 135 barabara za changarawe na kilometa 554 zikiwa ni barabara za udongo ambapo zaidi ya shilingi milioni 337 zimetumika kujenga madaraja na milioni 324 kujenga vivuko lengo ni kuweza kukabiliana na changamoto ya miundombinu ndani ya jiji la Arusha.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: