Na,Jusline Marco:Arusha
Kamati ya siasa Mkoa wa Arusha imetembelea na kukagua miradi mbalimbali katika sekta ya elimu, afya pamoja na miundombinu ya Barabara katika Wilaya ya Aruneru na kuridhishwa na kazi iliyofanyika.
Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Arusha Bw. Moloiment Olemoko akiwa mgeni rasmi katika ziara hiyo amesema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo imezingatia ila Ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na maelezo yanayotolewa na serikali ya awamu ya sita iliyopo chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassani.
Bw .Olemoko ametembelea mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Enaboishu Academy yenye mchepuo wa kingereza,mradi ulio gharimu shilingi million 20 na laki 4,lakini pia ametembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Olorien uliogharimu shilingi million 450 hadi kukamika kwake.
Kamati ya siasa ya Mkoa ilipofika katika shule ya msingi Enaboishu Academy kukagua ujenzi wa madarasa .
Olemoko amesema kamati hiyo amefurahishwa na ukamilikaji wa miradi hiyo kwa wakati na kwa kuzingatia bajeti iliyotengwa na serikali ambapo fedha hizo zimetokana na mapato ya ndani ya halmashauri yanayotokana na kodi za wananchi.
Aidha amesema licha ya miradi hiyo kukamilika ,bado mradi wa kituo cha afya cha Mwandeti haujakamilika kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara na ukosefu wa maji ambapo wameiomba serikali kuwatatulia changamoto hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango katika ziara hiyo amesema juhudi za serikali ya awamu ya sita ni kupanua wigo wa vyumba vya madarasa pamoja na kuongeza vituo vya afya katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango akizungumza katika ziara ya kamati ya siasa ya Mkoa iliyotembelea miradi inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita.
Katika hatua nyingine Mhandisi Ruyango amewaomba waalimu kuwa wabunifu katika kuwafundisha watoto kwa bidii kwa kuwa taifa linapambana na ujinga, umaskini na maradhi hivyo wanapaswa kuwapatia watoto elimu bora itakayo likomboa taifa hapo baadae na kuwaomba wananchi kutunza miundombinu hiyo ili iweze kutumiwa na vizazi vijavyo.
Amesema kuwa serikali ya awamu hiii imewekeza fedha nyingi katika idara ya Elimu ambapo katika Wilaya ya Arumeru imetoa fedha za kujenga madarasa 170 ambapo amesema kuwa kufuatia ilani ya chama cha Mapinduzi CCM serikali imetoa shilingi bilioni 2.4 za ujenzi wa miundombinu ya barabara katika wilaya hiyo.
Kwa upande wake mwalimu Mkuuu wa shule ya Sekondari Kimyanki Paschal Ginana ameishukuru serikali kuu kwa kuwekeza nguvu nyingi kwenye sekta ya elimu.
Post A Comment: