Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Samia Suluhu kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ujenzi meli ya MV Mwanza ili kurahisisha usafiri na usafirishaji katika mikoa inayozunguka Ziwa Viktoria na nchi Jirani.

Akizungumza baada ya kukagua na kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo jijini Mwanza, Mwenyekiti Seleman Kakoso amesema Serikali ya Awamu ya tano imeendelea kutoka fedha ili kuendeleza mradi huo ambapo dhamira hiyo itakuza pato la Mkoa na Serikali baada ya mradi kukamilika.

“Naipongeza sana Serikali hasa Mhe Rais sababu taarifa tuliyopewa hap ani kuwa Mkandarasi ameshalipwa Certificate zote alizowasilisha  kilichobaki ni sisi kama watanzania kujiweka tayari kwa meli hiyo itakapokamilika Amesema Mwenyekiti Kakoso.

Mwenyekiti Kakoso ameeleza umuhimu wa kuzingatia mahitaji ya rasilimali watu hasa kwenye taasisi zenye miradi mikubwa na kusisitiza kuwa uwepo wa watumishi wa kutosha kwenye kada muhimu kamai uhandisi na manunuzi kutaongeza tija na uzoefu kuanzia mwanzo wa miradi mpaka uendeshaji  wa miradi inapokamilika.

Aidha Mwenyekiti Kakoso ameitaka Wizara kusimamia Taasisi zinazofanya kazi kwa karibu ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Kampuni ya Huduma Meli (MSCL) na Shirika la Reli ya Tanzania (TRC) ili kuhakikisha mipango ya taasisi hizo inakwenda pamoja ili kuepuka kupishana kwenye utekelezaji wa miradi.

Naye Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, amemuhakikishia Mwenyekiti wa Kamati hiyo na wajumbe kuwa tayari Serikali imeshatoa maelekezo kwa taasisi hizo kushirikiana ili miradi itakapokamilika kusiwe na visingizio kwenye uendeshaji.

Naibu Waziri Mwakibete ameeleza kuwa pamoja na juhudi mbalimbali zinazoendelea tayari Kampuni ya Huduma za Meli, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Reli Tanzania (TRC) zimeshatiliana saini makubaliano maalum ya kusafirisha mizigo ikiwa ni moja ya jitihada ya ushirikiano.

Kamati ya Miundombinu iko Mkoani Mwanza kuakagua miradi ya WIzara ya Ujenzi na Uchukuzi.

(Imetolewa na KItengo cha Mawasiliano Serikalini, WIzara ya Ujenzi na Uchukuzi)
Share To:

Post A Comment: