Na mwandishi Wetu

Mkurugenzi wa kampuni ya  Viola Car Hire,Violet Mfuko pamoja na wenzake  Leo Machi 5  amekabidhi vifaa mbalimbali kama mashuka,maji , sabuni na maziwa vyenye thamani ya sh,10 milioni  katika   hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha (Mt Meru ) katika kilele cha kuelekea kwenye  maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Akikabidhi misaada hiyo mkurugenzi huyo alisema kwamba yeye pamoja na wafanyabiashara wenzake wameamua kujitolea faida wanayoipata na kuamua kujitolea misaada hiyo kama njia ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.


"Natoa wito kwa wafanyabiashara tusisite kuijali jamii yetu kwa kujitolea faida wanayoipata katika bias hatsa zao kuwajali wenzetu wenye mahitaji hususani wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali mbalimbali nchini hii ni thawabu kwao" Mkurugenzi wa kampuni ya Viola Car Hire ,Violet Mfuko


Naye katibu wa hospitali hiyo Angela Kimathi alisema kwamba uongozi wa hospitali hiyo unashukuru kwa misaada hiyo ambapo itakwenda kuwasaidia wakinamama waliojifungua na wale wajawazito.

"Tunashukuru sana kwa msaada huu kwa kuwa hii ni Mara ya pili sasa unajitolea sisi tunahaidi kuifikisha kwa walengwa waliokusudiwa" alisema Kimati

Naye ,Ally Bananga ambaye ni miongoni wadau waliojitolea vifaa hivyo alisema kwamba ni jambo jema kuwakumbuka wagonjwa walio hospitalini kwa kuwa baadhi yao wanapitia changamoto katika vifaa mbalimbali vya kujifungulia.

"Viola na sisi tulikuwa na uwezo wa kwenda kuzitumia fedha hizi kwenye matumizi mengine na starehe lakini tuliona ni jambo jema kuja kuwafariji hawa wagonjwa " alisema Bananga

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: