Na,Jusline Marco;Arusha


Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameipitisha rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa mwanachama ndani ya umoja huo uliokuwa unaundwa na nchi sita.


DRC imepitishwa leo Jumanne  katika mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa wanachama uliofanyika kwa njia ya mtandao chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.


Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo iliyo na idadi ya watu wanaofikia milioni 90 na inayopakana na nchi tano za jumuiya, iliomba kujiunga na taasisi hiyo ya kikanda mnamo Februari, 2021.


Katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Peter Mathuki amesema kujiunga kwa DRC na EAC kuna faida kubwa kiuchumi,kisiasa na kiulinzi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani kutaongeza fursa za kuichumi na kibiashara katika kusafirisha bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.


Jumuiya ya Afrika Mashariki tayari ilipitisha itifaki ya soko la pamoja,umoja wa forodha na sasa inaelekea katika itifaki ya sarafu moja na shirikisho la kisiasa ambapo katika uchumi soko la Jumuiya liliongezeka watu milioni 190 na kufikia takribani watu milioni 250 na kufanya kuwa miongoni mwa jumuiya kubwa kikanda.


Hata hivyo kujiunga kqa DRC Congo  kumepelekea  kupanuka kwa nchi wanachama na kupelekea kuwepo kwa nchi 7 katika Jumuiya hiyo ambapo mbali na Congo DRC ni Burundi,Kenya,Rwanda,Tanzania,Uganda na Sudan Kusini.

Share To:

Post A Comment: