Na,Jusline Marco:Arusha


Bodi ya Maji Bonde la Pangani limeendelea na zoezi la upandaji miti katika vyanzo vya maji vilivyomo chini ya Bodi hiyo Mkoani Arusha kwa lengo la kuhifadhi maji na kuvifanya vyanzo hivyo kuwa endelevu kwa vizazi vijavyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi hiyo Godwin Kapama amesema kuwa upandaji huo wa miti ambao ni endelevu umekuwa ukifanyika katika vyanzo vya maji ambavyo vina changamoto kubwa katika masuala mazima ya uhifadhi na utunzaji wake.

Aidha Kapama ameeleza kuwa Jumuiya za watumia Maji katika vyanzo hivyo zimekuwa zikizidiwa na uharibifu huo wa vyanzo kutokana na wananchi wenyewe kutotii sheria zilizopo hivyo ameiomba ushirikiamo kutoka kwa serikali ili kuhakikisha vyanzo vyote vya maji wanavilinda na kuviweka katika hali ya usalama.

Akizungumza katika moja ya zoezi la upandaji miti lililofanyika kwenye Chemchemi ya Moivaro, Kata ya Ambureni Wilayani Arumeru ambapo kilimo cha Salad ndani ya chanzo chenyewe,uoteshaji wa majani ya kulishia mifuho na ujenzi wa nyumba kumeleta athari kubwa katika chanzo hicho ilihali wananchi hao wanajua athari za uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji.

"Kampeni hii ambayo tumeianza tangu wiki ya maji kwa kupanda miti katika vyanzo mbalimbali tutaendelea nayo hadi msimu wa mvua zitakapoisha malengo yetu ni kupanda miti takribani laki 1 kwahiyo kwa kuhifadhi hili eneo tutaweza kuongeza kiasi cha maji ambacho kitakwenda kuhudumia idadi kubwa ya wananchi katika ukanda wa chini."Alisema Kapama Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Pangani

Awali Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango katika uzinduzi wa zoezi hilo la upandaji miti amewataka wananchi waliopanda salad hizo na kujenga nyumba zao katika chanzo hicho kuondoa mara moja ili kupisha chanzo hicho cha maji kuwa katika hali ya usalama ambapo pia amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru kufuta vibali holela vya viwanja katika eneo la chanzo cha maji ikiwa ji pamoja na kuwachukulia hatua wote waliohusika na ugawaji huo qa viwanja.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jimuiya ya watumia maji ya Mto Nduruma,Maliak Joel  amewataka wanasiasa kutohusisha suala la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji na siasa kwani suala la maendeleo ya wananchi ikiwrko utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira halihitaji siasa.


Naye Gurisha Sifael Mfanga katibu wa CCM Wilaya ya Arumeru amewataka wananchi wa kata ya Amburen  kufuata maagizo yote yanayotolewa na viongozi wao ili kuweza kuleta tija katika kata hiyo kupitia vyanzo vya maji.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ambureni Faraja Maliak amesema kuwa maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru watayatekeleza kwa mujibu wa sheria kwa kuondoa shughuli zote zinazoharibu vyanzo vya maji na kuwataka wananchi kuwa sehemu ya utunzaji wa vyanzo hivyo.

















Share To:

JUSLINE

Post A Comment: