Waandishi wa Habari wametakiwa kuimarisha weledi wao kwa kuandika habari zenye mantiki na kuleta tija kwenye jamii ikiwemo habari za uchunguzi na zile zinazoendana na mabadiliko ya tabia ya nchi.


Wito huo umetolewa na  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Andersh Sjoberg alipoitembelea Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kagera (KPC)  kwa ziara ya siku moja  Februari 25, 2022 kwa lengo la kukagua shughuli za utekelezaji na maendeleo ya Klabu hiyo.


Huu ni mwendelezo wa Balozi Sjoberg kuzitembelea Klabu za Waandishi wa Habari nchini ambazo ziko chini ya Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (UTPC), kila awapo na uratibu wa shughuli za kitaifa katika Mkoa husika.

Share To:

Post A Comment: