Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amezielekeza Taasisi za TANROAD, TARURA, DAWASA NA TANESCO kuhakikisha wanaboresha utoaji wa huduma ili kupunguza Kero na usumbufu kwa Wananchi.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao Cha pamoja na Viongozi wa Taasisi hizo kilicholenga kuwakumbusha suala la utoaji wa huduma Bora kwa Wananchi.

Kuhusu suala la Barabara, RC Makalla ameelekeza TANROAD/TARURA kuhakikisha Ujenzi wa Barabara za mwendokasi unaoendelea hauathiri Shughuli za maendeleo akitolea mfano Barabara za viwanda zilizofungwa na kusababisha viwanda kushindwa kufanya kazi ambapo ameshauri Busara itumike, pawepo na Matoleo na baadhi ya Shughuli zifanyike usiku.

Aidha RC Makalla ameelekeza Taasisi hizo kusimamia kikamilifu Ujenzi wa Barabara na kuhakikisha zinakamilika kwa wakati.

Hata hivyo RC Makalla amewataka TANESCO kuhakikisha wanafikisha huduma ya umeme kwenye maeneo ya pembezoni ikiwemo Chanika huku akitaka maboresho kwenye kitengo Cha mawasiliano.

Pamoja na hayo RC Makalla amewaelekeza DAWASA kumpatia taarifa ya miradi inayotekelezwa na hatua iliyofikia ili aweze kuikagua na Ile iliyokamikika izinduliwe.

RC Makalla pia ameendelea kuzitaka kila Taasisi kuhakikisha zinalinda maeneo yao yasivamiwe upya na Wafanyabiashara.

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: