JESHI la Polisi Iringa, limefanikiwa kukamata fedha  zaidi ya Sh Bilioni 1.07 pamoja na magari matano mapya ambavyo kwa pamoja vilipatikana kupitia wizi wa zaidi ya Sh Bilioni 2.1 mali ya kampuni ya Selecom Paytech Ltd.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi Allan Bukumbi amesema leo Ijumaa Feb 11, 2022 kuwa fedha hizo ziliibwa kupitia wakala wa Selcom wa mkoani Iringa, Tyson Kasisi ambaye ni miongoni mwa watuhumiwa wengine tisa, jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata.

“Wakala huyo kwa kupitia huduma ya Selcom Pay isivyo halali alihamisha fedha kwenda namba mbalimbali za simu na kisha kuchukua fedha taslimu kupitia wakala wa huduma za kifedha za mitandao mbalimbali ya simu pamoja na akaunti za benki,” amsema.

Amesema wizi huo ulifanyika kwa njia ya mtandao katika maeneo ya mkoa wa Iringa, Dar es Salaam na Morogoro kati ya Novemba 9 na 27 mwaka 2021 baada ya wakala huyo kufanikiwa kuchezea mfumo wa kielektroniki wa Selcom Pay unaomilikiwa na kampuni hiyo ya Selcom Paytech Ltd.

Share To:

Post A Comment: