Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na Viongozi na Wataalam wa Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam katika Kikao Kazi cha Mikakati na Kampeni ya Kuhamasisha Shughuli za Ukuzaji Viumbe Maji Bahari kilichofanyika Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani Februari 24, 2022. Mhe. Ulega aliwahimiza Viongozi hao kuwahamasisha Wananchi wao kuchangamkia fursa zilizopo katika uchumi wa buluu ikiwemo ufugaji wa Kaa, Majongoo Bahari, Kambakochi na ukulima wa Mwani.

 Na Mbaraka Kambona, Pwani

NAIBU  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewahimiza Viongozi wa Mikoa iliyopo Pwani ya Bahari ya Hindi hususan Pwani na Dar es Salaam kuhamasisha wananchi wao kujiunga katika vikundi vya ushirika ili wawezeshwe na serikali kunufaika na fursa zinazopatikana katika uchumi wa buluu ikiwemo ufugaji wa kaa, majongoo bahari na kilimo cha mwani.

Ulega alitoa rai hiyo katika kikao kazi cha mkakati wa kampeni ya kuhamasisha shughuli za ukuzaji viumbe maji bahari kwa viongozi na wataalam wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kilichofanyika Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani Februari 24, 2022.

Alisema ili wananchi waweze kunufaika na fursa hizo, suala la kuwa na ushirika ni muhimu sana huku akihimiza kila halmashauri kuhamasisha wananchi kujiunga katika vikundi na kuunda ushirika katika maeneo yao.

“Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hotuba yake aliyoitoa Januari 7, 2022 katika kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar alisisitiza shughuli za ukuzaji viumbe maji hususani ufugaji wa kaa kuwa ni moja ya fursa za ajira kwa vijana”,alisema Mhe. Ulega

Alifafanua kwa kusema kuwa Ibara ya 43 (h) ya Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi inahimiza kuanzishwa vikundi vya ushirika vya wavuvi na wafugaji viumbe maji huku akiongeza kuwa kukuza na kuimarisha uchumi wa buluu ni moja ya kipaumbele cha serikali ya awamu ya sita, hivyo ni muhimu kuwaanda wananchi na fursa pana iliyopo katika tasnia ya ukuzaji viumbe maji ili serikali inapoanza kuwawezesha wawe wako tayari.

Aidha, alisema Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji katika kuzitumia fursa hizo zikiwemo mitaji midogo ya uwekezaji, upatikanaji wa pembejeo mbalimbali na masoko ya baadhi ya mazao yatokanayo na ukuzaji v

iumbe maji, katika kukabiliana na changamoto hizo,alisema, mwaka 2019, Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilianzisha Dawati la Sekta Binafsi ili liwe kiunganishi au daraja kati ya Wizara, wawekezaji, masoko na taasisi za kifedha kama njia mojawapo ya ufumbuzi wa tatizo la mitaji, masoko na vitendea kazi kwa wavuvi, wakuzaji viumbe maji.

Lengo la ziara yake ni kutathmini na kufanya kikao kazi cha kuweka Mikakati na kampeni ya kuhamasisha kutumia ipasavyo fursa za uchumi wa buluu


Share To:

Post A Comment: